MSANII LINAH AJIFUNGUA MTOTO WA KIKE
MSANII LINAH AJIFUNGUA MTOTO WA KIKE
Mwimbaji wa muziki wa kizazi kipya, Estelina Sanga maarufu kama Linah amejifungua mtoto wa kike salama katika hospitali ya Marie Stopes, Mwenge jijini Dar es Salaam.
Linah amejifungua leo, Jumanne, Julai 25 ikiwa ni muda mfupi baada ya maneno ya mashabiki zake kusambaa kwamba ujauzito wake ni wa muda mrefu tofauti na ilivyo kawaida.
Mtu wa karibu na msanii huyo amesema kuwa mama na mtoto kiafya wanaendelea vizuri.
Hata hivyo katika kipindi chote cha ujauzito wake, Linah amekuwa akimtaja mpenzi wake wa sasa anayejulikana kwa jina moja la Shaban kwamba ndiye baba wa mtoto wake.
Miaka kadhaa nyuma, Linah amewahi kuzungumzia kuhusu taarifa za kuharibika kwa ujauzito wake wa kwanza ambao ulikuwa wa mpenzi wake wa zamani
Comments
Post a Comment