MKATABA wa kipa wa Azam FC, Aishi Salum Manula kusaini Simba umevuja kwenye mitandao ya kijamii na unaonyesha mlinda mlango huyo amesaini kwa dau la Sh. Milioni 50 kwa miaka miwili na atakuwa analipwa Milioni 3 kwa mwezi mshahara. Hata hivyo, mkataba huo unasema, Aishi atalipwa kwa awamu fedha hizo, Sh. Milioni 25 wakati wa kusiani, Milioni 5 kabla ya Agosti 30 na Sh. Milioni 20 atamaliziwa kabla ya Desemba mwaka huu. Aishi anakuwa mchezaji wa pili tegemeo wa Azam FC kuhamia Simba SC, baada ya aliyekuwa Nahodha wa timu hiyo ya Chamazi, John Raphael Bocco kutangulia pia Msimbazi kwa dau la Sh. Milioni 50 miaka miwili na mshahara wa Sh. Milioni 4 kwa mwezi. Wachezaji wote wanaondoka Azam FC wakati mikataba yao inamalizika mwishoni mwa mwezi huu na mazungumzo ya kusaini mikataba mipya yalishindikana, kutokana na sera mpya za timu ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake kutotumia fedha nyingi katika kusajili. Aishi aliyesimama langoni jana katik...
Comments
Post a Comment