Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA) na Rais wa Chama cha Mawakili Tanzania, Mhe. Tundu Lissu ameachiwa kwa dhamana ya Milioni 10 leo katika kesi yake iliyokuwa inamkabili ya uchochezi.Mahakama ya Kisutu imempa dhamana Mh Tundu Lissu kwa sharti la kuwa na wadhamini wawili watakaosaini dhamana ya thamani ya milioni kumi.
Aidha, Mahakama hiyo pia imemtaka Tundu Lissu kutokuondoka nje ya jiji la Dar es Salaam bila kuwa na kibali maalum cha mahakama. Uamuzi huo umetolewa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam, Wilbard Mashauri.
Upande wake Tundu Lissu alikuwa anatetewa na jopo la mawakali 18 likiongozwa na Fatma Karume na Peter Kibatala ambapo katika shauri la kwanza waliomba Mahakama impe dhamana mteja wao.
Tundu Lissu alitiwa katika mikono ya dola mnamo Julai 20 siku ya Alhamsi katika uwanja wa ndege akiwa anaelekea nchini Rwanda. na siku iliyofuata jeshi hilo lilikwenda kufanya upekuzi nyumbani kwa Mbunge huyo.
Aidha kesi yake imepangwa kusikilizwa Agosti 24 mwaka huu baada ya wadhamini wake kukamilisha taratibu zote za kumdhamini.
Comments
Post a Comment