UKWELI KUHUSU MZEE MAJUTO, NA TETESI ZA KUFA
MSANII wa filamu nchini, Haji Salum maarufu kama Mboto, amekanusha taarifa zinazosambaamitandaoni zinazodai kuwa nguli wa vichekesho katika tasnia ya uigizaji, Amri Athuman maarufu kama King Majuto amefariki dunia.
Mboto baada ya kupata taarifa hizi alifunga safari kuelekea
mkoani Tanga ambapo ni nyumbani kwaMzee Majuto na kumkuta hai, na amekanusha uvumi huo kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuposti picha inayowaonyesha yeye na Majuto wakiwa nyumbani kwake, na picha hiyo iliambatana na maneno yafuatayo:
“Baada ya kupata taarifa mbaya kuhusu Mzee Majuto nimelazimika kuja kwake Tanga. Ni kweli anaumwa ila anaendelea vizuri na si kama watu walivyozusha kuwa mzee hatunaye. Kwa sasa mzee ni mzima nipo naye Tanga,” ameandika Mboto.
Siku chache zilizopita, gazeti la Ijumaa Wikienda liliripoti taarifa za kuumwa kwa Mzee Majuto, anayesumbuliwa na tatizo la ngiri, lakini jana kwenye mitandao ya kijamii zikaenea taarifa zisizo za kweli kwamba King Majuto amefariki dunia.
Comments
Post a Comment