ALICHOSEMA WAZIRI UMMY BAADA YA KUFANYA ZIARA KITUO CHA AFYA MATEI, KALAMBO

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amewataka watoa  huduma za afya katika kituo cha afya cha Matei wilayani Kalambo kutoa huduma bora kwa wanawake wajawazito
Rai hiyo imetolewa jana na Waziri huyo alipokuwa kwenye ziara ya kikazi wilayani hapo na kutembelea hospitali hiyo pamoja na kuongea na watumishi wa sekta ya afya kujua changamoto zinazowakabili
Alisema wajawazito wanapaswa kupata huduma bora kila wanapofika kliniki kila mwezi kwa kuangaliwa mfano dalili za kifafa cha mimba ,wigi wa proteini pamoja na viatarishi vingine  vinavyoweza kusababisha  uzazi pingamizi na hivyo kupelekea vifo kwa mama au mtoto wakatiwa kujifungua
“Nawapongeza sana kwa kutenga dirisha la wazee ila kusiwepo tu dirisha bali muwape dawa wazee wasio kuwa na uwezo,hivyo kama kuwakatia mfuko wa bima ya jamii (CHF)ni gharama basi wapatieni vitambulisho vya matibabu bure ili wazee wakija kwenye matibabu wasije na barua za watendaji wa vijiji,” alisema Ummy.
Kwa upande wa madawa Waziri Ummy amewaambia watendaji hao hakuna masharti magumu ya ununuzi wa madawa na vifaa tiba kwa kutumia pesa za CHF“nimeshawaambia MSD ndani ya masaa ishirini na nne umeagiza vitu MSD hana,ndani ya masaa hayo kama hana unaruhusiwa kwenda kununua unapotaka kwenda”hivyo ni vyema wakapitisha wadhaburi watakaokuwa wananunua.
“Tangu serikali hii iingie madarakani imefanya mabadiliko makubwa katika upatikanaji wa dawa kwa kuongezwa bajeti ya dawa kwa asilimia kubwa hizi changamoto ndogondogo zipo ila mwisho wa siku wananchi wanahitaji dawa,hivyo kuhakikisha dawa zile muhimu zinapatikana wakati wote.” alisema Ummy.
Hata hivyo amewataka kuwapa kipaumbele wale wanaotumia bima ya afya,nataka kuona mnaongeza wananchi watakaotumia bima ya afya kwenye matibabu ili kuweza kutatua changamoto za sekta ya afya
Upande wa Malaria Waziri Ummy vipimo vya haraka vya malaria vya MRTD ni bure pamoja na dawa ya kutibu Malaria’ALU’ ni bure ”asije kuwaambia mtu kipimo hicho utoe pesa,sindano kama mtu amezidiwa na maralia kali ni bure,” alisisitiza Waziri Ummy
Akiongelea ugonjwa wa Kifua Kikuu”TB” Waziri huyo alisema ni wakati wa kuwaambiwa watu Tb inatibika kwani katika kila watu mia moja wanaoumwa kifua kikuu na kutumia dawa watu tisini wanapona kabisa na wanaendelea na shughuli zao.

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi