Liverpool wacharaza Hoffenheim 4-2 na kufuzu Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya

Emre Can akifungia Liverpool

Haki miliki ya picha
Image captionMjerumani Can alifunga mabao yake ya kwanza msimu huu


Ushindi wao dhidi ya Hoffenheim umehakikisha kwamba kwamba mara ya kwanza England itawakilishwa na klabu tano katika hatua ya makundi Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Liverpool walionyesha mchezo mkali wa kushambulia na kuwazidi nguvu wapinzani wao katika michuano ya muondoano ya kufuzu kwa hatua ya makundi Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Jumatano na kuondoka na ushindi wa 4-2, na jumla ya 6-3.
Liverpool walikuwa wakiongoza 2-1 kutoka kwa mechi ya kwanza na walihakikisha mambo hayawezi kuwageuka kwa kufunga mabao matatu dakika 20 za kwanza za mechi.
Emre Can aliwafungia la kwanza kabla ya Mohamed Salah kuongeza la pili.
Can alifunga la pili kutoka kwa krosi ya Roberto Firmino sekunde 143 baadaye kabla ya nguvu mpya wa Hoffenheim Mark Uth, aliyeingizwa dakika ya 24 kuokoa jahazi la klabu hiyo ya Ujerumani kukomboa bao moja.
Mshambuliaji wa zamani wa Hoffenheim, Firmino, hata hivyo alihakikisha Liverpool wanaibuka wababe kwa kufunga baada ya mapumziko Jordan Henderson alipompokonya mpira nahodha wa wapinzani wao Kevin Vogt.
Wajerumani hao, ambao walimaliza wa nne katika Bundesliga msimu uliopita, hawakufa moyo na waliokomboa bao jingine Sandro Wagner alipofunga kwa kichwa kutoka kwa krosi ya Andrej Kramaric.

Jurgen KloppHaki miliki ya picha
Image captionMeneja wa Liverpool Jurgen Klopp awali aliongoza Dortmund Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mara nne

Liverpool pamoja na Chelsea, Tottenham, Manchester City na Manchester United watawafahamu wapinzani wao hatua ya makundi Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya droo itakapofanywa baadaye leo Alhamisi saa moja jioni saa za Afrika Mashariki (17:00 BST).

Liverpool's Sadio ManeHaki miliki ya pich
Image captionSadio Mane ameanza kutekeleza mchango muhimu tena uwanjani Anfield na aliwafaa sana dhidi ya Hoffenheim.

Mechi ya Liverpool ijayo?
Mechi ijayo ya Liverpool itakuwa katika Ligi ya Premia - na ni mechi kubwa.
Baada ya kwenda mechi mbili za kwanza bila kushindwa, kwa kutoka sare na Watford na kulaza Crystal Palace, watakuwa wenyeji wa Arsenal uwanjani Anfield siku ya Jumapili (16:00 BST).

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi