Muathiriwa wa shambulizi la Septemba 11 atambuliwa baada ya miaka 16

Scene of attack




Haki miliki ya picha

Muathiriwa mwingine wa shambulizi la Septemba 11 mwaka 2001 kwenye jumba la World Trade Center mjini New York ametambuliwa.
Muathiriwa huyo wa kiume ni mtu wa 1,641 kutambuliwa kati ya watu 2,753 ambao waliuawa wakati wa shambulizi hilo.
Kutambuliwa huko kulikofanywa kwa kutumia teknolojia ya DNA kumewekwa siri kwa ombi la familia.
Kabla ya tangazo hilo la siku ya Jumatatu, imechukua zaidi ya miaka miwili tangu mtu wa mwisho atambuliwe.
Muathiriwa wa mwisho alitambuliwa mwezi machi mwaka 2015.
Jumla ya watu 1,112 waliouwawa wakati huo, asilimia 40 bado hawajatumbuliwa karibu miaka 16 baada ya shambulizi hilo la kigaidi.
Ndege mbili ziligonga majengo mjini New York na moja katika jengo la Pentagon huko Virginia na nyingine huko Pennsylvania, na kuua karibu watu 3000 na kuwajeruhi maelfu.

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi