PICHA: KATIBU MKUU WA WIZARA YA AFYA ALIVYOSHIRIKI UJENZI WA ZAHANATI IRINGA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Sihaba Nkinga ameshiriki ujenzi wa zahanati ya Ufyemba iliyopo kata ya Wasa mkoani Iringa ili kuhamasisha wananchi kufanya kazi kwa maendeleo.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akihamasisha wananchi kuendeleza ari ya kushiriki kazi za maendeleo ya kijiji chao cha Ufyemba mkoani Iringa kwa kushirikiujenzia wa zahanati hiyo ambayo unajengwa na wananchi wa kijiji hicho kwa kutumia nguvu za wananchi wenyewe ili kusogeza huduma za afaya kijijini.
Wananchi wa kijiji cha Ufyemba wakishiriki katika kubeba matofali na kujenga jingo la zahanati ya kijiji hicho ili kuondokana na taatizo la kutembea umbali mrefu kutafuta huduma za afya.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga akikabidhi mifuko 50 ya saruji kwa Mwenyekiti wa Kijij cha Ufyemba Bw Ronaganius Lunyungu ili kuunga mkono jitihada za wananchi hao katika kukamilisha ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Ufyemba.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga akikabidhi pesa kwa Mwenyekiti wa Kijij cha Ufyemba Bw Roganius Lunyungu zilizopatikana katika harambee ili isaidie katika kumalizia Ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Ufyemba.
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Ufyemba wakifurahia ujio wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga(hayupo pichani) alipofanya ziara ya kushiki kwa vitendo kazi za miradi ya maendeleo iliyoibuliwa na kutekelezwa kwa kutumia nguvu za wananachi wenyewe katika kijiji hicho. (Picha na Erasto Chin’goro, Iringa)
Comments
Post a Comment