Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 30.08.2017
Tottenham wanakaribia kukamilisha usajili wa beki wa kimataifa wa Argentina Juan Foyth, 19, kutoka Estudiantes kwa pauni milioni 8 na pia bado wanajaribu kumsajili beki wa PSG Serge Aurier, 24, kwa pauni milioni 23. (Guardian)
Liverpool wamekubali kumuuza kiungo Philippe Coutinho, 25, kwenda Barcelona kwa pauni milioni 148. (Yahoo Sports)
Jose Mourinho anataka kumsajili winga wa Leicester City Riyad Mahrez. (SFR Sport)
Arsenal huenda wakashawishiwa kumuuza Alexis Sanchez, 28, iwapo watapata dau la kuvutia. (BBC Radio 5 live)
Arsenal wamekataa dau la pauni milioni 30 kutoka Liverpool la kumtaka Alex Oxlade-Chamberlain, ambaye pia amekataa kwenda Chelsea kwa pauni milioni 40. (Evening Standard)
Raheem Sterling atabakia Manchester City na hatokuwa sehemu ya mkataba wa City kumsajili Alexis Sanchez kutoka Arsenal. (Sky)
Sergio Aguero huenda akataka kuondoka Manchester City mwezi Januari iwapo Pep Guardiola ataendelea kutomtumia. (Manchester Evening News)
Inter Milan wamepanda dau jipya kumtaka beki wa kati wa Arsenal Shkodran Mustafi, 25. (Sky Sports)
Tottenham wanafikiria kutopanda dau la kutaka kumsajili kiungo wa Everton Ross Barkley, 23, kwa sababu ni majeruhi kwa sasa. (London Evening Standard)
Arsenal wamepanda dau la kutaka kumsajili winga wa Real Madrid Lucas Vazquez. (Diario Gol)
Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa huenda akashangaza wengi na kujiunga na Las Palmas kwa mkopo huku akisubiri kujiunga na Atletico Madrid. (Sun)
Dau la pauni milioni 25 la Chelsea kumtaka Ross Barkley limekataliwa na Everton. (BBC)
Beki wa kati wa West Brom Jonny Evans, 29, atakataa kujiunga na Arsenal na badala yake anataka kwenda Manchester City. (Daily Mail)
West Brom wanatarajia kumsajili beki wa kati Grzegorz Krychowiak, 27, kutoka Paris Saint-Germain. (Sun)
West Brom pia wanatarajia kukamilisha usajili wa beki wa Arsenal Kieran Gibbs, 27, katika saa 24 zijazo. (Daily Mirror)
Beki wa Southampton Virgil van Dijk, 26, bado ana matumaini ya kwenda Liverpool ingawa Arsenal na Chelsea huenda nazo zikapanda dau katika saa za mwisho kabla ya dirisha la usajili kufungwa. (Independent)
Crystal Palace watamuunga mkono meneja wake Frank de Boer kwa kusajili wachezaji watatu wapya. (Daily Star)
Stoke City wanataka kumsajili kiungo wa Manchester City Fabian Delph, 27, na wapo tayari kutoa pauni milioni 12, kwa mchezaji huyo aliyenunuliwa kwa pauni milioni 8 kutoka Aston Villa miaka miwili iliyopita. (Daily Telegraph)
Meneja wa Newcastle United Rafael Benitez yuko tayari kumuuza mshambuliaji wake Dwight Gayle, 26, kwa pauni milioni 18. (Guardian)
Napoli wanataka kumsajili kiungo wa Barcelona Denis Suarez, 23. (Corriere dello Sport)
Winga Adama Traore, 21, anataka kuondoka Middlesbrough kwenda Lille. (Gazette Live)
Divock Origi huenda akaondoka Liverpool na kwenda Tottenham, kwa mujibu wa baba yake. (Sky)
Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii (Kwa Kiingereza): Uhamisho wa wachezaji Ulaya
Comments
Post a Comment