Chama cha mawakili Kenya chamkosoa Uhuru Kenyatta

Rais wa LSK Isaac Okero


Haki miliki ya pichaFACEBOOKK
Image captionRais wa LSK Isaac Okero

Chama cha mawakili nchini Kenya LSK kimemkosoa rais Uhuru Kenyatta wa Kenya dhidi ya kuwashambulia majaji wa mahakama ya juu kufuatia uamuzi wa kubatilisha uchaguzi wake.
Rais wa LSK Isaac Okero katika taarifa siku ya Jumamosi alimkosoa rais Kenyatta kwa kumtaja jaji mkuu David Maraga na majaji wengine wa mahakama hiyo kuwa ''wakora''.
Rais Kenyatta alitoa matamshi hayo wakati wa ziara ya kukutana na wafuasi wake katika soko la Burma mjini Nairobi siku ya Ijumaa muda mfupi baada ya mahakama hiyo ikiongozwa na jaji Maraga kufutilia mbali uchaguzi wake.
Bwana Okero alisema: Matamshi ya rais kwamba majaji hao wasubiri rais Uhuru Kenyatta achaguliwe katika uchaguzi ujao hayafai kutoka kwa kiongozi wa taifa ambaye chini ya katiba ya Kenya ni nembo ya umoja wa Wakenya.
Amesema kuwa rais Kenyatta anapaswa kulinda haki ya majaji na idara yote ya mahakama.
Bwana Okero amesema kuwa ijapokuwa rais huyo ana haki ya kutoa maoni yake anafaa kutoa maoni yanayostahiki.
''Haki yake inafaa kuheshimu, kukubali na kulinda haki za jaji mkuu na kila jaji wa mahakama ya juu chini ya kifungu cha sheria cha 28''.
''Matamshi hayo yanakiuka na yanashutumiwa na chama cha mawakili Kenya LSK'', aliongezea.
Kiongozi huyo wa LSK amesema kuwa mahakama hiyo ilifanya wajibu wake na kuwaonya viongozi wengine dhidi ya kuwatishia majaji.
Mahakama ya juu inayoongozwa na jaji Maraga ilifutilia mbali ushindi wa rais Uhuru Kenyatta kutokana na dosari iliotekelezwa na tume ya uchaguzi nchini Kenya IEBC.

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi