Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi
Mshambuliaji nyota wa Atletico Madrid na Ufaransa Antoine Griezmann ameomba radhi baada yake kushutumiwa vikali kwa kujipaka rangi nyeusi kama sehemu ya utani wa kubadilisha sura.
Alikuwa awali amewaambia wafuasi wake kwenye Twitter watulie kabla ya kulazimika kuchukua hatua hiyo.
Griezmann alikuwa amepakia kwenye Twitter picha yake akiwa amevalia kama mchezaji mweusi wa mpira wa kikapu.
Baadaye aliifuta picha hiyo, sawa na ujumbe wa pili aliokuwa ameuandika uliosema: "Tulieni nyote. Mimi ni shabiki wa Harlem Globetrotters na natoa heshima kwao."
Ujumbe wake wa tatu ulikuwa wa kuomba radhi.
Aliandika: "Natambua kwamba nilikowa kumakinika. Iwapo nimewakera baadhi ya watu, basi naomba radhi."
Mbunge wa chama cha Labour UIngereza David Lammy alikuwa miongoni mwa waliomshutumu Griezmann.
Aliandika kwenye Twitter: "Kuna njia nyingi sana za kujifurahisha kwenye sherehe, na si lazima upake uso wako rangi nyeusi.
"Siwezi kuamini kwamba tuko hapa 2017 tukiwakumbusha watu kwamba hawafai kujivalisha mavazi na kujifanya weusi."
Comments
Post a Comment