Moto wa nyika watishia mji wa Santa Barbara California
Shughuli mpya ya kuhamisha watu umeamrishwa baada ya moto mkubwa wa nyika kusini mwa jimbo la California kukosa kudhibitiwa siku ya Jumapili.
Ukichochewa na upepo moto huo wa nyika wa Thomas, unatishia mji wa pwani wa Santa Barbara na mwingine ulio karibu wa Carpinteria.
Wazima moto mapema walisema kwa kuwa moto huo ulikuwa unadhibitiwa lakini wakaongeza kuwa umeteketeza eneo lenye ukubwa wa jimbo la Chicago.
Licha ya moto mwingine katika jimbo hilo kudhibitiwa kwa sehemu kubwa, moto wa Thomas umedhibitiwa kwa asilimia 15 tu.
Amri ya kuhama imetowa usiku sehemu za Carpinteria karibu na msitu wa Los Padres kilomita 160 kutoka Los Angeles.
Watabiri walisema kuwa upepo unatarajiwa kuongezeka siku ya leo kabla ya kupungua tena usiku.
Idara ya moto ilichapisha picha zinazoonyesha ukisambaa kwenda kwa nyumba eneo la Carpinteria maea Jumapili.
Siku ya Jumamosi Gavana wa California Jerry Brown aliitaja hali hiyo kuwa mpya na kusema kuwa moto huo unaochochewa na mabadiliko ya hali ya hewa utatokea kila mwaka.
Moto wa sasa umewazimu kuhamishwa watu 200,000 kote katika jimbo hilo na kuharibi nyumba 800.
Wazima moto kadhaa wamejeruhiwa lakini ni mtu mmoja tu ameuwa.
Kuna hofu kuwa moto huo utaharibu sekta ya thamani ya mamilioni ya dola ya kilimo katika jimbo la Carlifonia.
Comments
Post a Comment