Cristiano Ronaldo apewa kadi nyekundu mechi ya El Clasico

Cristiano Ronaldo shown a red card


Haki miliki ya pich
Image captionCristiano Ronaldo alikosa mechi nyingi za kujiandaa kwa msimu baada ya kuchezea Ureno Kombe la Mabara

Cristiano Ronaldo alifunga bao lakini baadaye akafukuzwa uwanjani huku Real Madrid wakilaza Barcelona 3-1 katika Super Cup ya Uhispania, mechi ya mkondo wa kwanza.
Gerard Pique alijifunga kutoka kwa krosi ya Marcelo kabla ya Lionel Messi kusawazisha kupitia mkwaju wa penalti.
Ronaldo, aliyeingia kama nguvu mpya alirejesha Real Madrid mbele alipokimbia kutoka katikati ya uwanja na kufunga.
Alipewa kadi ya njano kwa kuvua shati lake kusherehekea.
Muda mfupi baadaye, alioneshwa kadi nyingine ya manjano kwa kujiangusha na akafukuzwa uwanjani.
Marco Asensio alifunga la tatu.
Ronaldo aliamini kwamba alifaa kupewa penalti baada yake kuanguka alipokabiliwa na Samuel Umtiti, na alionekana kumsukuma refa baada yake kuoneshwa kadi nyekundu.
Ronaldo alikaa dakika 24 pekee uwanjani.
Barcelona walionekana kutatizika bila Neymar ambaye alihamia Paris Saint Germain kwa rekodi ya dunia ya £200m.

Cristiano RonaldoHaki miliki ya picha
Image captionCristiano Ronaldo amefunga mabao 11 katika mechi 11 za karibuni alizochezea Nou Camp

Real watakuwa wenyeji wa Barca mechi ya marudiano Jumatano saa 22:00 BST (saa sita usiku saa za Afrika Mashariki).

Gerard DeulofeuHaki miliki ya pi
Image captionGerard Deulofeu alirejea Barcelona kutoka Everton

Barcelona walimchezesha Gerard Deulofeu safu ya mashambulizi pamoja na Lionel Messi na Luis Suarez.

Comments

Popular posts from this blog

GOR MAHIA MABINGWA WA SPORTPESA SUPER CUP 2017, SASA KUKIPIGA NA EVERTON JULAI 13

Marekani na Korea Kusini wafanya mazoezi ya pamoja ya jeshi

UKWELI KUHUSU MZEE MAJUTO, NA TETESI ZA KUFA