Marekani na Korea Kusini wafanya mazoezi ya pamoja ya jeshi

South Korean marines participate in landing operation referred to as Foal Eagle joint military exercise with US troops Pohang seashore on 2 April 2017 in Pohang, South Korea.


Haki miliki ya picha
Image captionKorea Kaskazini tayari imelaani mazoezi hayo ikisema kuwa hatua hiyo ni sawa na kumwaga mafuta kwenye moto.

Marekani na Korea Kusini wanafanya mazoezi ya kila mwaka ya jeshi, ambayo mara nyingi huighadhabisha Korea Kaskazini licha ya wito wa kutaka mazoezi hayo yasifanyike.
Wiki iliyopita Korea Kaskazini ilionekana kulegeza kamba baada ya kutisha kuwa itarusha makombora kwenda kisiwa cha Marekani cha Guam, lakini tena ikasema kuwa itafuatilia mienendo ya Marekani.
Korea Kaskazini tayari imelaani mazoezi hayo ikisema kuwa hatua hiyo ni sawa na kumwaga mafuta kwenye moto.

An F/A-18 fighter lands on the deck of the Nimitz-class aircraft carrier USS Carl Vinson during a South Korea-US joint military cxercise in seas east of the Korean Peninsula on 14 March 2017.Haki miliki ya picha
Image captionMazoezi hayo hujumuisha ya ardhini , baharini na angani

China na Urusi mwezi Julai zilipendekeza kusitishwa mazoezi ya kijeshi ili nayo Korea Kaskazini iache kuyafanyia majaribio makombora.
Marekani inasema kuwa mazoezi hayo yatawahusisha wanajeshi 17,500 wa Marekani na yatadumu kwa kipindi cha siku kumi.
Marekani na Korea Kusini hufanya mazoezi ya kijeshi mara mbili kwa mwaka yanayowashirikisha idadi kubwa ya wanajeshi na zana za kivita.

Emergency services personnel wearing protective clothing participate in an anti-terror and anti-chemical terror exercise as part of the 2016 Ulchi Freedom Guardian (UFG) at Yeoui subway station on August 23, 2016 in Seoul, South Korea.Haki miliki ya picha
Image captionMazoezi hayo ambayo hufanyika Korea Kusini pia hujumuisha mazoezi jinsi ya kukabiliana na ugaidi na mashambulizi ya kemikali.

Mazoezi hayo hujumuisha ya ardhini , baharini na angani. Mazoezi hayo ambayo hufanyika Korea Kusini pia hujumuisha mafunzo jinsi ya kukabiliana na ugaidi na mashambulizi ya kemikali.
Korea Kusini hutuma wanajeshi 50,000 huku Marekani nayo ikituma kati ya wanajeshi 25,000 na 30,000.
Mazoezi hayo pia wakati mwingine hushirikisha wanajeshi kutoka nchi washirika na mwaka uliopita nchi zingine tisa zilijiunga nayo.

US soldiers give first aid to a mock victim in a tent during a joint medical evacuation exercise as part of the annual massive military exercises, known as Key Resolve and Foal Eagle, at a South Korean Army hospital in Goyang, northwest of Seoul, on 15 March 2017.Haki miliki ya picha
Image captionMazoezi hayo ambayo hufanyika Korea Kusini pia hujumuisha mazoezi jinsi ya kukabiliana na ugaidi na mashambulizi ya kemikali.

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi