Marekani kuipiga Korea Kaskazini ikimgusa mshirika wake

Trump amesema Korea Kaskazini inajitafutia matatizo

Image captionTrump amesema Korea Kaskazini inajitafutia matatizo

Waziri wa masuala ya ulinzi wa marekani James Mattis amesema kuwa tishio lolote kutoka korea kaskazini kwa Marekani ama washirika wake litajibiwa vikali na jeshi.
Mattis amezungumza hayo baada ya mkutano wake na Rais Trump juu ya masuala ya usalama wa nchi kufuatia jaribio la nyuklia huko Pyongyang.
Trump ameonya kuwa Marekani inaweza kusimamisha kufanya biashara na nchi yoyote inayoshiriki biashara na Korea Kaskazini.
China ndio mshirika mkuu wa baishara na Pyongyang, ameongeza kuwa korea kaskazini imekua tishio na imeleta fedheha kwa Beijing.
Alivyoulizwa na waandishi wa habari kama Marekani itashambuliwa na korea kaskazini, rais trump alisema kuwa tutaona''
Nayo korea kusini imesema kuwa imefanya majaribio matano kama majibu ya jaribio la nyuklia la korea kaskazini.

Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, (katikati) akipokea maelekezo ya namna bomu hilo linavyofanya kazi
Image captionRais wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, (katikati) akipokea maelekezo ya namna bomu hilo linavyofanya kazi

Rais wa Urusi na Raisi wa china wote wamesisitiza juu ya umuhimu wa kuondokana mzozo wa Korea.
Nao Japan wamesema kuwa jaribio hilo si la kusamehewa.
Jaribio hilo ni la sita kufanywa na kore kaskazini katika kipindi cha miaka 10.
Limesababisha tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.3 lilifika katika mkoa wa china uliokaribu na Korea Kaskazini.

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi