Posts

Showing posts from January, 2018

Tetesi za Soka Ulaya Jumanne.

Image
Haki miliki ya picha AFP Image caption Henrikh Mkhitaryan Arsenal wako makini kumsaini kiungo wa kati wa Manchester United Henrikh Mkhitaryan 28, kama sehemu ya makubaliano ambayo yatamleta mshambuliaji raia wa Chile Alexis Sanchez, 29, huko Old Trafford. (Guardian) Manchester City wamejitoa katika makubaliano ya kumsaini Sanchez na pesa zilizoitishwa na ajenti wake. (Goal) Refa amrushia teke mchezaji kisha kumpa kadi Ufaransa Arsenal ilifanya mazungumzo na mshambuliaji wa Bordeaux Malcom siku ya Jumapili na wanatarajia kulipa pauni milioni 40 kwa mBrazil huyo wa miaka 20. (Guardian) Arsenal na Chelsea wanammezea mate mshambuliaji wa Watford raia wa Brazil Richarlison 20. (Sun) Haki miliki ya picha PA Image caption Andy Carroll Chelsea bado wako makini kumsaini mshambuliaji wa mwezi Januari kwa mkopo huku Andy Carroll wa West Ham akiwa katika nafasi nzuri wa kusainiwa. (Telegraph) Manchester United wako tayari kumpa kipa wa miaka 27 David de Gea mkataba mpya amboa ...

Watu 20 wameuawa katika mapigano Libya

Image
Haki miliki ya picha AFP Image caption Mashambulizi yanayofanywa Libya Watu 20 wameuawa kufuatia mapigano yaliyotokea kati ya makundi ya wanamgambo hasimu katika mji mkuu wa Libya, Tripoli. Mapigano hayo yamesababisha kusitishwa kwa safari za ndege, katika uwanja wa kijeshi wa Maitiga, ambao ndio wa pekee wa kimataifa mjini Tripoli. Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters ndege zipatazo tano zimeathiriwa na mapigano hayo. Seikali ya Maridhiano ya kitaifa ya Libya imesema shambulio hilo ni jaribio la kundi moja la wapiganaji kuachiliwa kwa wafuasi wake waliokuwa wakishikiliwa na kundi wanalopingana nalo. Ghasia za mara kwa mara zimekuwa zikitokea mjini Tripoli tangu mweaka 2011.

Watoto waliofungwa minyororo wapatikana kwenye nyumba California

Image
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption David Allen Turpin, 57, na Louise Anna Turpin, 49, walikamatwa kwa mashtaka ya mateso na kuhatarisha maisha ya watoto. Wazazi wawili wamekamatwa huko California baada ya polisi kupata watu 13 waliokuwa wameshikiliwa mateka nyumbani kwao wakiwemo wengine waliofungiwa kwa vitanda vyao kwa minyororo na vifuli. David Allen Turpin, 57, na Louise Anna Turpin, 49, walikamatwa kwa mashtaka ya mateso na kuhatarisha maisha ya watoto. Watu hao 13 walio na umri wa kati ya miaka miwili na 29, walipatikana kwenye nyumna huku Peris kilomita 95 kusini mashariki mwa Los Angeles. Wote hao wanaaminiwa kuwa ndugu. Maafisa waligungua hilo siku ya Jumapili wakati mmoja wa watu hao alifanikiwa kuponyokana na kupiga namba ya dharura akitumia simu ambayo alipata ndani ya nyumba. Msichana huyo ambaye polisi wanasema alionekana kuwa na umri wa miaka 10, alidai kuwa ndegu zake wengine 12 walikuwa wakishikiliwa na wazazi wao. Polisi baadaye walipat...