Watoto waliofungwa minyororo wapatikana kwenye nyumba California

David Allen Turpin (left) and Louise Anna Turpin


Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionDavid Allen Turpin, 57, na Louise Anna Turpin, 49, walikamatwa kwa mashtaka ya mateso na kuhatarisha maisha ya watoto.

Wazazi wawili wamekamatwa huko California baada ya polisi kupata watu 13 waliokuwa wameshikiliwa mateka nyumbani kwao wakiwemo wengine waliofungiwa kwa vitanda vyao kwa minyororo na vifuli.
David Allen Turpin, 57, na Louise Anna Turpin, 49, walikamatwa kwa mashtaka ya mateso na kuhatarisha maisha ya watoto.
Watu hao 13 walio na umri wa kati ya miaka miwili na 29, walipatikana kwenye nyumna huku Peris kilomita 95 kusini mashariki mwa Los Angeles.
Wote hao wanaaminiwa kuwa ndugu.
Maafisa waligungua hilo siku ya Jumapili wakati mmoja wa watu hao alifanikiwa kuponyokana na kupiga namba ya dharura akitumia simu ambayo alipata ndani ya nyumba.
Msichana huyo ambaye polisi wanasema alionekana kuwa na umri wa miaka 10, alidai kuwa ndegu zake wengine 12 walikuwa wakishikiliwa na wazazi wao.
Polisi baadaye walipata watoto kadhaa wakiwa wamefungiwa kwa vitanda vyao kwa nyororo na vufuli gizani katika mazingira yenye harufu mbaya.
Lakini wazazi hawakuweza kutoa sababu juu ni kwa nini watoto hao walifungwa kwa njia kama hiyo.
Polisi walishangazwa kugundua kuwa saba kati ya wale waliokuwa wakizuiliwa kwenye nyumba hiyo walikuwa ni watu wazima wa kati ya umri wa miaka 18 na 29.
Waathirirwa walioneka kuwa na afya mbaya na wachafu.
Waathiriwa hao wote kwa sasa wanatibiwa kweny hospitali za eneo hilo.

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi