Posts

Watu 235 wauawa katika shambulio la msikiti Misri

Image
Haki miliki ya picha EPA Image caption Wanamgambo waliulenga msikiti mmoja karibu na eneo la al-Arish Wanamgambo wametekeleza shambulio la bomu na ufyatuaji wa risasi katika msikiti mmoja uliopo kaskazini mwa eneo la Sinai na kuwaua takriban watu 235 kulingana na chombo cha habari cha taifa. Walioshuhudia wanasema kuwa msikiti wa al-Rawda katika mji wa Bir al-Abeid , karibu na al-Arish ulilengwa wakati wa ibada ya Ijumaa. Maafisa wa polisi wanasema kuwa wanaume wanne waliokuwa ndani ya gari moja waliwafyatulia risasi waliokuwa wakiabudu kulingana na chombo cha habari cha AP. Misri imekuwa ikikabiliana na wanamgambo katika eneo hilo tangu 2013. Kumekuwa na mshambulio ya mara kwa mara yanayolaumiwa kutekelezwa na wanamgambo katika rasi ya Sinai lakini hilo ni shambulio baya zaidi kuwahi kufanyika. Picha katika eneo la mkasa huo zinaonyesha damu iliomwagika ndani ya msikiti. Image caption Ramani ya eneo la al-Arish Takriba watu 125 walijeruhiwa ripoti zinasema. Ripo...

Mugabe na mkewe wasusia sherehe ya kuapishwa kwa Mnangagwa

Image
Image caption Rais Mugabe na mkewe Grace Mugabe walisusia sherehe ya kuapishwa kwa Emmerson Mnangagwa Robert Mugabe na mkewe Grace walikosa kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwa rais Emmerson Mnangagwa baada ya wananiasa hao kukubaliana kwamba Mugabe anaweza kupumzika. Sababu kuu ilioteolewa ni kwamba bwana Mugabe alikuwa amechoka. Mugabe na mkewe Grace hawajaonekana hadharani tangu kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 93 kujiuzulu kama rais kufuatia shinikizo kutoka kwa jeshi na raia. Hatua hiyo inajiri baada ya Mugabe na mkewe kufumta kazi rais huyo mpya wakati alipokuwa makamu wa rais kwa madai kwamba alikuwa akipanga njama za kutaka kumuondoa madarakani rais Mugabe Aliyekuwa makamu wake wa rais Emmerson Mnangagwa amewataka raia wa Zimabwe kusalia watulivu na kuweka amani na kutolilipiza kisasi. Umati mkuwa wa takriban raia 60,00 wa Zimbabwe wakiwemo viuongozi wa kimataifa na wanadplomasia walihudhuria sherehe ya kumuapisha Mnangagwa katika uwanja wa michezo wa mj9ini h...

Emmerson Mnangagwa ni nani?

Image
Image caption Mfahamu rais mpya wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa Bwana Emerson Mnangagwa amekuwa mwandani wa Robert Mugabe kwa karibu miaka 40 tangu na hata kabla Zimbabwe kujipatia uhuru wake. Bwana Mnangagwa mwenye umri wa miaka 75 amekuwa karibu zaidi na Mugabe tangu enzi zile wakiwa jela walipokamatwa kutokana na harakati zao za kupigania na katika shughuli nzima za mapambano ya kuikomboa Zimbabwe. Bwana huyo alizaliwa tarehe 15 septemba mwaka 1942 kabla ya babake kuhamia nchini Zambia alikoanza harakati za mapambano. Safari yake ya kufikia hadi sasa anaapishwa kuwa rais wa Zimbabwe imekuwa ya utaraibu lakini ya kiuhakika. Uhuru ulipopatikana , bwana Mugabe hakumsahau rafiki yake alimchaguwa kuwa waziri wa Usalama wa kitaifa .  Lakini baadae aliteuliwa kushikilia nyadhifa mbali mbali katika serikali ya rafiki yake na babake wa kisiasa - Robert Mugabe. Lakini safari yake hadi kufikia kuchagulikwa kuwa naibu rais mwaka 2014 haikuwa rahisi . Kuna wakati alipokuk...

Mnangagwa aapa kuwahudumia raia wote wa Zimbabwe

Image
Image caption Mnangagwa akichukua kiapo cha kuwa rais Raia wa Zimbabwe wamekusanyika kwa wingi kwenye uwanja wa michezo mjini katika mji mkuu wa nchi hiyo Harare kwa ajili ya sherehe za kuapishwa kwa rais mpya wa nchi hiyo Emmerson Mnangagwa.  Mnangagwa ameapishwa kama rais wa Zimbabwe, kufuatia kuondoka kwa rais kuondoka kwa Robert Mugabe madarakani baada ya miaka 37 ya utawala wa kiimla. Emmerson Mnangagwa, kwa jina la utani The the crocodile", ameanza hotuba yake kama rais wa Zimbabwe. ''Nahisi furaha sana kwa uamuzi wa chama cha Zanu PF kunialika kuhudumia taifa letu la Zimbabwe kama rais na kamanda mkuu wa majeshi kuanzia leo''. ''Sina ujuzi wa kazi hii lakini nitawahudumia wananchi wote bila upendeleo wa rangi ama kabil''a. Amemsifu Robert Mugabe kwa kupiginia uhuru huku akisema kuwa alichukua uongozi wakati mgumu . Amesema kuwa licha ya makosa yaliofanywa na Mugabe ni muhimu kukubali na kutambua mchango wake kuhusu ujenzi wa...

Robinho: Mshambuliaji wa Brazil ahukumiwa kwenda jela kwa ubakaji

Image
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Robinho aliifungia Brazil mabao 28 katika michezo 100 Mchezaji soka wa Brazil Robinho amehukumiwa kifungo cha miaka tisa jela kwa kushiriki katika genge lililombaka mwanamke mmoja mjini Milan mwaka 2013. Mahakma ya Italia imesema kuwa Robinho mwenye umri wa miaka 33- na raia wengine wa Brazil walimbaka mwanamke raia wa Albania , aliekuwa na umri wa miaka 22, baada ya kumnwesha pombe kwenye kilabu cha usiku mjini Milan. Mchezaji huyo wa safu ya ushambuliaji, aliyeondoka katika klabu ya AC Milan mnamo mwaka 2015 baada ya kuichezea miaka mitano hakuwepo mahakamani wakati wa hukumu hiyo lakini alikana mashataka dhidi yake kupitia wakili wake. Hukumu hiyo haitatolewa hadi pale mchakato wa rufaa utakapokamilika.  Robinho, aliichezea Manchester City na sasa anachezea timu ya Atletico Mineiro nchini Brazil. Ujumbe kwenye ukurasa wa Instagram wa Robinho unasema "tayari amekwisha jitetea dhidi ya shutuma, akisisitiza kuwa hakus...

Balozi wa Angola, Tanzania amtaka Eduardo dos Santos kushtakiwa

Image
Haki miliki ya picha AFP Image caption Balozi wa Angola, Tanzania amtaka Eduardo dos Santos kushtakiwa Balozi wa Angola nchini Tanzania amemtaka rais wa zamani wa taifa hilo Jose Eduardo dos Santos kushtakiwa kwa madai ya uhalifu aliyotekeleza wakati wa utawala wake wa miaka 38. Ambrosio Lukoki amesema kuwa bwana dos Santos anafaa kujiuzulu kama kiongozi wa chama tawala cha MPLA kwa kuwa alikuwa anatumia wadhfa wake huo kuzuia kushtakiwa. Rais mpya wa Angola Joao Lourenco hivi majuzi aliwafuta kazi wakuu wa polisi na vitengo vya ujasusi ,hatua iliokiuka sheria kwamba hatofanya hivyo kwa kipindi cha miaka minane. Pia alimfuta kazi mwanawe bwana Dos Santos ambaye ni bilionea kama mkuu wa kampuni ya mafuta ya taifa hilo. Bwana Lourenco kwa jina la utani JLo alichaguliwa na bwana Santos kusimama katika uchaguzi wa mwezi Agosti na wakati huo wachaganuzi walidhani kwamba ataendeleza uongozi wa bwana Santos.

Dr Slaa aliyekuwa kiongozi wa upinzani ateuliwa kuwa balozi

Image
Image caption Dkt Wilbord Slaa alikuwa katibu mkuu wa chama cha upinzani CHADEMA Aliyekuwa Katibu mkuu wa chama cha upinzani CHADEMA ameteuliwa kuwa balozi na Rais wa Tanzania, John Magufuli. Katika taarifa ilitolewa na Mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu ,Gerson Msigwa, haijataja kituo chake cha kazi. Ila imeeleza "ataapishwa baada ya taratibu kukamilika" Dokta Wilbord Slaa alikuwa kiongozi muandamizi wa upinzani nchini Tanzania. Alijiuzulu nafasi ya ukatibu mkuu na uanachama wa Chadema mwaka 2015 baada ya ujio wa waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa ambaye alipewa nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho mwaka huo. Slaa amekuwa katika siasa kwa zaidi ya miongo miwili na kabla ya hapo alikuwa padri wa kanisa katoliki.