Majambazi 27 wenye silaha wakamatwa mkoani Pwani
Majambazi 27 wenye silaha wakamatwa mkoani Pwani
Jeshi la polisi Mkoa wa Pwani limefanya msako mkali katika mapori mbali mbali na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wa ujambazi 27 pamoja na risasi 153,bunduki 2 mabomu 3 ambavyo walikuwa wakivitumia katika matukio ya uharifu.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Kamishina mwandamizi
Jafari Ibrahimu amesema kwamba watuhumiwa hao wamekamatwa baada ya
kufanyika operesheni katika magenge yaliyopo vichakani na kuwakuta
watuhumiwa hao wakiwa wamejificha pamoja na silaha walizokuwa wanazitumia
kufanyia uhalifu
Ameongeza kuwa wameamua kufanya operesheni hiyo kutokana
na kuongezeka kwa uharifu katika baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Pwani na
kuwakamata watuhumiwa hao ambao wengine walikutwa na vifaa mbali mbali
ikiwemo visu mapanga,pamoja na nyaya tatu za milipuko ya mabomu.
Katika zoezi hilo pia waliweza kukamata madawa ya kulevya aina aya
bangi gunia 18 na mirungi kilo 124,lita 88 za pombe ya moshi pamoja na
mitambo yake mitatu ya kutengenezea noti bandia 370 na meno ya tembo.
Comments
Post a Comment