ZIJUE FAIDA ZA MBEGU ZA MABOGA
Mandai
Herbalist Clinic hapa inakufahamisha baadhi ya faida za mbegu za
maboga, lakini kwanza ni vizuri ifahamike kuwa mbegu za maboga hutokana
na tunda liitwalo boga,
tunda ambalo asili yake haifahamiki vizuri ni wapi, ingawaje baadhi ya
tafiti
zinasema kuwa asili yake ni Amerika ya kaskazini.
Zao la maboga mara nyingi hushamiri zaidi katika
msimu wa joto na inashauriwa kupanda zao hili mwanzoni mwa mwezi Julai hasa
katika udongo unaotunza maji vizuri.
Hata hivyo zao hili huweza kuathirika endapo
kutakuwa na upungufu wa maji au joto dogo sana, lakini pia zao hili huweza
kuathirika linapopandwa katika udongo ambao hauchuji maji vizuri.
Lakini tukiachana na hayo ni vizuri ifahamike kwamba
mbegu za maboga zinafaida nyingi sana kiafya na hujumuisha kiwango kingi cha
protini na vitamin, huku ikiaminika kwamba, mbegu hizo huweza kupunguza mafuta
kwenye mishipa ya damu na jambo la msingi zaidi ni kwamba gramu moja ya mbegu
za maboga huwa na protini sawa na glasi moja ya maziwa.
Watu wengi wanaweza kudharau mbegu za maboga pengine
kwa kutokufahamu faida zake, lakini wazi kwamba mbegu hizi ni miongoni mwa
mbegu zenye faida kubwa mwilini, kwani huweza kuzuia na kutibu hata baadhi ya
magonjwa hatari yaliyoshindikana hospitalini.
Zifuatazo
ni faida za kiafya ambazo mtu anaweza kuzipata kwa kula mbegu za maboga zikiwa
mbichi au zilizo kaangwa:
Huimarisha
moyo na mifupa
Mbegu za maboga huwa kiwango kingi cha madini aina
ya magnesium, ambayo ni muhimu kwa afya ya moyo na uimarishaji wa mifupa pamoja
na mishipa ya damu sambamba na kuongeza
ufanisi wa utumbo mpana . Magnesium inaonesha uwezo mkubwa wa kuzuia mshtuko wa
moyo na kiharusi.
Kinga
ya mwili
Mbegu za maboga zina kiwango cha madini aina ya
zink, ambayo pia yana faida nyingi mwilini ikiwa ni pamoja na na uimarishaji wa
kinga mwilini , ukuaji wa seli, macho na ngozi ya mwili. Hali kadhalika zinki huimarisha
nguvu za kiume.
Saratani
ya kibofu
Kutokana na kuwa na kiwango kingi cha zinki, tafiti
zinaonesha kuwa mafuta ya mbegu zenyewe za maboga huweza kutumika kama dawa ya
kutibu saratani ya kibofu.
Ugonjwa
wa ini
Mbegu za maboga pia zina kamba lishe na kinga kubwa
ya kupambana na magonjwa nyemelezi. Mbali na hayo mbegu hizi zina virutubisho
vinavyotoa kinga dhidi ya magonjwa ya ini na moyo.
Usingizi
Kwa watu wenye matatizo ya kukosa usingizi,
wanashauriwa kula punje kadhaa pamoja na tunda lolote muda mfupi kabla ya kupanda kitandani, utafiti umeonesha
kwamba mbegu za maboga zina kirutubisho kinachohamasisha uzalishaji wa homoni
za usingizi kwa wingi
Uvimbe
Mbegu za maboga zimeonesha kuwa na virutubisho vingi
vyenye uwezo wa kuzuia magonjwa yote ya uvimbe mwilini, ikiwa ni pamoja na
kuvimba miguu, vidole na hata majipu.
Mambo
ya kuzingatia
Hakikisha unakula mbegu ambazo hazijaoza na zilizo
safi na ambazo hazijakaa muda mrefu, lakini pia tumia mbegu hizo kwa usalama
zaidi ikiwa ni sambamba na kuziosha na maji safi na salama kisha zianike na
inapendeza zaidi ukila bila kukaanga, lakini ukila pia baada ya kukaanga bado
utapata faida zake. Isipokuwa hakikisha haziungui wakati unapozikaanga unaweza
kutumia dakika 10 tu katika zoezi hilo la kuzikaanga.
Unaweza fika kituoni kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam endapo una tatizo lolote la kiafya.
BY Dr Mandai
Comments
Post a Comment