Trump aapa kuwa atashinda vita Afghanistan

Trump amesema ataongeza idadi ya wanajeshi Afghanistan


Image captionTrump amesema ataongeza idadi ya wanajeshi Afghanistan

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa kuondolewa kwa wanajeshi wa Marekani kutoka nchini Afghanistan kutaacha pengo ambalo huenda likajazwa na magaidi.
Alisema kuwa mapango yake ilikuwa ni ya kuondoa vikosi vya Marekani, lakini badala yake ameamua wanajeshi hao kubakia ili kuzuia kurudia makosa ambao yalitokea nchini Iraq.
Amesema pia kuwa anaongeza idadi ya wanajeshi watakao pelekwa nchini Afghanstan.
Akizungumza kupitia Televishen, Rais Trump amesisitiza kuwa kipaumbele cha Marekani ni kutekeleza masuala yenye maslahi katika usalama wa taifa hilo, kutokomeza mtandao wa ugaidi.

Trump amesema ni vigumu kuwaondoa wanajeshi wa Marekani nchini humo
Image captionTrump amesema ni vigumu kuwaondoa wanajeshi wa Marekani nchini humo

Amesisitiza pia kuwa kitendo cha Marekani kujiondoa kwa haraka Afghanistan, kitatatoa mwanya kwa ugaidi kujiimarisha zaidi kama ilivyotokea Iraq.
Hata hivyo Trump amekwepa kuzungumzia moja kwa moja muda wa mwisho wa ushiriki wa Marekani nchini Afghastan na idadi kamili ya ongezeko la wanajeshi.
Rais Trump ameitupia lawama Pakistan kwa madai kuwa inawahifadhi magaidi ambapo amesema suala hilo linapaswa kuachwa mara moja.
Katika hatua nyingine amezungumzia mpango wa Marekani kuimarisha mpango wa ushirikiano na India.

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi