Uchaguzi Kenya: Matokeo kamili ya urais yasubiriwa
- Ni siku ya tatu sasa tangu Wakenya walipofika katika vituo vya kura kuwachagua viongozi na matokeo kamili ya uchaguzi wa urais yanaendelea kusubiriwaTume ya Uchaguzi inaendelea kupokea Fomu 34A za matokeo ya urais kutoka vituoni
- Matokeo ya awali yanaonesha Rais Kenyatta anaongoza akiwa na kura 8 milioni. naye Bw Odinga ana kura 6.6 milioni.
- IEBC imesema mitambo yake haidukuliwa, kinyume na madai ya muungano wa upinzani Nasa
- Jumanne kulitokea vurugu katika baadhi ya maeneo mtaa wa Mathare, Nairobi na baadhi ya maeneo Kisumu. Lakini kwa sasa hali ni tulivu
- Waziri wa usalama Fred Matiang'i amewaomba wananchi kuendelea na shughuli za kawaida bila wasiwasi
- Katika barabara za Nairobi magari yameanza kuonekana lakini bado hali ya kawaida haijarejea
Hivi ndivyo magazeti nchini Kenya yalivyoangazia matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika Jumanne, hatua ya upinzani kupinga matokeo ya awali yanayotangazwa, kutokea kwa maandamano katika baadhi ya maeneo na hali ilivyo kwa jumla nchini humo:
Comments
Post a Comment