Wafikishwa mahakamani Uganda kwa mauaji

Polisi nchini Uganda

Haki miliki ya pichaUGANDA POLICE
Image captionPolisi nchini Uganda

Watu 12 wamefikishwa mahakamani nchini Uganda kwa mashtaka ya mauaji ya wanawake tisa katika eneo la kaskazini nje ya mji mkuu Kampala.
Kati ya washtakiwa hao wawili ni wanawake.
Wote kwa pamoja wanashtakiwa kwa makosa ya ugaidi na wizi wa kutumia nguvu.
Jumla ya wanawake 19 wameuawa katika maeneo ya mji wa Kampala tangu mwezi Mei.
Wengi kati yao walikuwa wamebakwa na kukatwa viungo vyao, huku miili yao ikiachwa porini na pembezoni mwa barabara.
Mkuu wa polisi nchini Uganda amesema imani za kishirikina zinahusishwa katika baadhi ya mauaji.

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi