Zanzibar kunani??Simba nayo yawasili Unguja, Yanga yatimkia Pemba kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Hisani

Mchezaji wa timu ya Simba ya Dar  aliyesainiwa kutoka wahasimu wa jadi Yanga, Haruna Nyiyonzima alipowasili katika Bandari ya Unguja jana mchana

 Wachezaji wa timu ya Simba ya Dar walipowasili katika Bandari ya Unguja jana mchana
 Kocho Mkuu wa timu ya Simu Omog akiwa akisubiri usafiri wa kuwapeleka Hoteli ya Mtoni Marine watakaapofikia  wakati walipowasili katika Bandari uya Unguja jana mchana

Wachezaji wa timu ya Simba ya Dar walipowasili katika Bandari ya Unguja jana mchana

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Kikosi cha wachezaji 23 cha Simba kimewasili Visiwani Zanzibar jioni ya leo wakitokea Jijini Dar es salam kwaajili ya kuweka kambi Mjini Unguja wakijiandaa na mchezo wao wa Ngao ya Hisani dhidi ya Yanga ambao nao leo asubuhi waliondoka Unguja na kwenda Pemba kwaajili ya kambi pia.

Simba wataweka kambi visiwani hapa mpaka Agosti 22, 2017 siku moja kabla ya mchezo wao utakaopigwa Agosti 23 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salam.

Simba watafanya mazoezi kwenye uwanja wa Amaan ambapo watatarajiwa kucheza michezo miwili ya kirafiki visiwani hapa kujipima nguvu.

Kambi ya Simba ipo kwenye Hoteli ya Mtoni Marine iliyopo Maruhubi Mjini Unguja.

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi