Makamu wa Rais apongeza juhudi za MERCK nchini Tanzania



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan  amezipongeza juhudi zinazofanywa na taasisi ya Merck ambayo ni kampuni inayoongoza katika sayansi na teknolojia  ambayo imelenga  kushughulikia masuala  uwezeshwaji wa wanawake na huduma za afya akisema kwamba wamekuja nchini  kwa wakati mwafaka


Wakati wa mkutano maalum kati ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Merck Foundation  Makamu wa Rais  alisema kuwa Merck Foundation  inakaribishwa na serikali inatarajia kushirikiana  na taasisi hiyo  inayoheshimika na iliyo makani katika  kuwezesha wanwake , vijana, huduma za afya  na sayansi.

Tunatambua mchango  unaotolewa na Merck Foundation  katika kujengea uwezo  huduma za afya barani Afrika na tunakaribisha shughuli zake  nchini Tanzania, hususani katika kampeni zinazolenga  kuuongezea umma  uelewa kuhusu ugumba.

Makamu wa Rais aliongeza, “Mimi binafsi nitafanya kazi na Merck katika kuwawezesha wanawake walio na uwezo duni kijamii na kiuchumi kote nchini Tanzania  na sehemu nyingine duniani ili kujenga utamaduni mpya  katika kuheshimu na kumtambua wanawake  kama sehemu ya wanajamii wanaozalisha  wawe ni kinamama na hata wasio wazazi.”

Merck Foundation hali kadhalika imejikita  katika ushirikiano wa muda mrefu na serikali ya Tanzania katika kuijengea uwezo katika huduma za afya  na kuboresha kufikiwa kwa  ubunifu na masusluhisho  yaliyo katika uwiano  kote nchini ikiwa ni sehemu ya  program za uwajibikaji kwa jamii barani Afrika.

“Merck Foundation itatilia mkazo katika uwezeshwaji wa wanawake walio na tatizo la ugumba  kupitia upatikanaji wa taarifa, uelewa, afya, kubadili mitazamo na kuwewawezesha kiuchumi kote nchini  kupitia kampeni ya Merck ya Zaiidi ya mama,” alisema Ofisa Mtendaji Mkuu wa Merck, Dk. Rasha Kelej.

Kampeni hiyo ambayo inatoa msukumu kwa vyombo vya habari na wadau wengine  kuchpisha na kuwasilisha mada kwa njia ya mtandao, video na vipindi vya redio kuhusu masuala yanayohusu ugumba ilizinduliwa nchini Tanzania Juni mwaka huu. Washindi katika kampeni hiyo  wanatarajiwa kuondoka  na zawadi ya fedha  kuanzia dola 1000 hadi dola 5000.

 “Tatizo la ugumba barani Afrika ni kubwa, inakadiriwa kuwa  mtu mmoja kati ya kila watu wane walio na umri wa kuzaa anasumbuliwa na tatizo la  ugumba, na takribani  asilimia 85 wale walio na tatizo la ugumba linatokana na ukosefu wa tiba kwa ugonjwa ambao unaweza kutibika,  hivyo kuongeza uelewa  kuhusu kuzuia hali hiyo  kupiti vyombo vya habari vya ndani na mitandao ya jamii ni hatua muhimu.”, alisema Dk. Rasha Kelej’’

Aliongeza, “Kujenga uelewa  kuhusu ugumba kwa wanaume kwani ugumba  una athari sawa kwa wanaume na wanawake, lakini wamekuwa ndio  wanaolaumiwa  peke yao, wanatengwa na kudhalilishwa ndani ya jamii zao. Kampeni itashughulikia mada hizi na kutoa msukumo kwa wanaume  kujadili kwa uwazi  tatizo lao la ugumba  na kushirikiana  katika safari ya kutambua ugumba na matibabu ya wake zao.”

 Kwa upande mwingine Merck foundation itajikita zaidi katika kugharamia mafunzo kwa wataalamu wa afya kwenye maeneo ya saratani kwa watoto (paediatric oncology) katika programu za udhamini nchini India, Ulaya na katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwa madaktari wa Tanzania ili kuboresha upatikanaji wa huduma zote zinahusu saratani.

Hivi karibuni Merck ilizindua Tuzo ya Kuvitambua Vyombo vya Habari kupitia kampeni yake ya “Zaidi ya Mama” ili kuwatuza waandishi wa habari na wanafunzi wanaosomea uandishi wa habari katika eneo la Afrika Mashariki ambao watakuwa wamefanya vizuri katika  kuandika  habari zinazoelewesha, kuelimisha na  kuhabarisha  ambazo zitaweza kujenga jukwaa  la majadiliano kuhusu ugumba ndani ya Afrika. Hafla ya kutoa tuzo hizo inatarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu 2017.

Lengo la tuzo hizo  ni kujenga uelewa kuhusu mchango muhimu ambavyo vyombo vya habari vinaweza kuutoa  katika  kuondo unyanyapaa uliojikita katika tatizo la ugumba. Hali kadhalika  zinalenga  utamaduni mbovu wa kuwabagua na kuwadhalilisha wanawake na papo hapo kuuelimisha umma  kuhusu kuzuia ugumba, kuisimamia hali hiyo na  ugumba kwa wanaume. Nyongeza katika kampeni hiyo ni kwamba inalenga kutoa msukumo kwa wanawaume  kujadili hali yao ya ugumba kwa uwazi, kuwasaidia wake zao katika safari zao za kupimwa na  kutibiwa.

Kufahamu zaidi kuhusu program za Merck Foundation na mafunzo yao pamoja na fursa za udhamini. Tafadhali tembelea tovuti yao www.merck-foundation.com na www.merckmorethanamother.com

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi