Marekani yadai kuwasiliana na Korea Kaskazini ''moja kwa moja''

Rais Xi Jinping wa China na waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Rex Tillerson


Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionRais Xi Jinping wa China na waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Rex Tillerson

Marekani inawasiliana na Korea Kaskazini ''moja kwa moja'', kulingana na waziri wa maswala ya kigeni Rex Tillerson.
Bwana Tillerson alisema kuwa Washington ilikuwa unachunguza uwezekano wa mazungumzo na Pyongyang, ''kwa hivyo subirini''.
''Tunawasiliana na Pyongyang'', alisema wakati wa ziara ya China.Hatuko katika hali mbaya''.
Korea Kaskazini na Marekani zimekuwa zikirushiana cheche za maneno katika miezi ya hivi karibuni lakini haikujulikana kwamba walikuwa wakiwasiliana.
Rais wa Marekani Donald Trump ametishia kuiangamiza Korea Kaskazini , akisema kiongozi wa taifa hilo Kim Jong-Un, ''anahatarisha maisha yake'' hatua iliomshinikiza rais huyo wa Korea Kaskzini kutoa taarifa akiapa kumnyamazisha kwa vita rais huyo wa Marekani aliyemtaja kuwa ''mtu mwenye akili punguani''.
Korea Kaskazini iliendeleza cheche hizo za maneno siku ya Jumamosi , ikitoa taarifa iliomtaja rais Trump kuwa mzee mwenye akili punguani anayehatarisha maisha yake kwa kuitisha shambulio la nyuklia ambalo litaiangamiza Marekani.
Cheche hizo za maneno zinajiri kufuatia majaribio ya mara kwa mara ya makombora na Pyongyang inasema kuwa mnamo Septemba 3 ilifanikiwa kulifanyia majaribio bomu la hydrogen linaloweza kuwekwa katika kombora la masafa marefu.
Majaribio hayo yalishutumiwa na jamii ya kimataifa , huku Umoja wa Mataifa ukiiwekea vikwazo Korea Kaskazini kwa lengo la kuishinikiza kusitisha utengezaji wa makombora.
Bwana Tillerson yuko nchini China akikutana na rais Xi Jinping na maafisa wengine akitumai kuwashawishi kutekeleza vikwazo hivyo.
Wiki hii China iliwaambia wafanyibiashara wa Korea Kaskazini wanaotekeleza operesheni zao ndani ya taifa hilo kufunga bishara zao.
Hatahivyo China bado inaunga mkono majadiliano na Korea Kaskazini.

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi