Man United yaibana Crystal Palace 4-0
Klabu ya Manchester United imeonyesha mchezo mzuri na kuweza kuicharaza Crystal Palace 4-0 na hivyobasi kuilazimu klabu hiyo kupoteza mechi yake ya saba msimu huu bila kufunga bao.
United ambao hawajapoteza waliongoza baada ya dakika tatu wakati Marcus Rashford alipowachanganya mabeki wa Palace na kutoa pasi nzuri kwa Juan Mata aliyecheka na wavu akiwa umbali wa maguu 10.
Bao la pili lilijiri baada ya Ashley Young kupiga krosi ambayo ilifungwa na Marouane Fellaini.
Fellaini alifunga bao la pili kupitia kichwa cha karibu kufuatia mkwaju wa adhabu uliopigwa na Rashford mapema katika kipindi cha pili.
Romelu Lukaku alifunga bao la nne kunako dakika za lala salama likiwa bao la 11 katika mechi 10 za United, kwa kumaliza krosi iliopigwa na Martial.
Matokeo hayo yanaipeleka United katika kilele cha jedwali kwa muda mchache huku Manchester United ikialikwa na Chelsea huko darajani.
Comments
Post a Comment