Polisi wachunguza vifo vingi vya watoto wanaozaliwa India
Polisi nchini India wanachunguza vifo vya watoto kadhaa wanaozaliwa kwenye hospitali ya Farrukhabad, huko Pradesh.
Watoto 49 walifariki katika hospitali ya Ram Manohar Lohia ndani ya mwezi mmoja wakiwemo 30 waliofariki kutokana na tatizo linalojulikana kama "perinatal asphyxia".
Hali hiyo inasababishwa na viwango vya chini vya hewa wakati wa kuzaliwa.
Mwezi Agosti takriban watoto 160 walifariki katika hospitali ya Gorakhpur katika jimbo hilo hilo.
Baadhi ya vifo vilitajwa kusababishwa na ukosefu ya hewa.
Lakini mafisa wa vyeo vya juu serikalini wamekana kuwa hiyo ndiyo sababu kutokea vifo kwenye hospitali zote.
Kwenye uchunguzi wa hivi majuzi ripoti ya serikali iliwalaumu madaktari kwa vifo vya watoto 30, na kusababisha kufanywa uchunguzi
Vivo vyote 49 vilitokea kati ya Julai 21 na Agosti 20.
Poisli walisema kuwa katika kisa cha Farrukhabad, hospitali haikuweka hewa kwa mipira ya watoto baada ya kuzaliwa.
Eneo hilo ni moja ya maeneo maskini zaidi nchini India na ushuhudia mamia ya vifo vya watoto kutokana na magonjwa tofauti.
Comments
Post a Comment