Utafiti: Kilimo cha kupindukia chanzo cha majangwa



Utafiti wa umoja wa mataifa umebaini kuwa thuluthi moja ya ardhi kote duniani imeharibiwa na shughuli nyingi za kilimo kupindukia


Image captionUtafiti wa umoja wa mataifa umebaini kuwa thuluthi moja ya ardhi kote duniani imeharibiwa na shughuli nyingi za kilimo kupindukia

Utafiti wa umoja wa mataifa umebaini kuwa thuluthi moja ya ardhi kote duniani imeharibiwa na shughuli nyingi za kilimo kupindukia
Utafiti huo unaonyesha kwamba udongo usiokuwa na rutuba unatishia kuzua baa la njaa kwa mamilioni ya watu pamoja na kuleta umaskini na mizozo.
Umoja wa mataifa unasema tani bilioni ishirini na tano za udongo wenye rutuba na miti bilioni kumi na tano hupotea kila mwaka.
Umesema kuwa sera za kitaifa za kuzuia ardhi kubadilika na kuwa jangwa ni muhimu katika kuzuia kile inachodai huenda kikawa chanzo cha migogoro lakini ukaongezea kuwa uhifadhi wa chakula pia unaweza kusaidia.
Utafit huo umebaini kwamba ukulima unaofanywa na viwanda ambapo mashine kubwa hutumiwa kulima na kuvuna hupunguza rutuba ya udongo kwa kiwango kikubwa.

Comments

Popular posts from this blog

GOR MAHIA MABINGWA WA SPORTPESA SUPER CUP 2017, SASA KUKIPIGA NA EVERTON JULAI 13

Marekani na Korea Kusini wafanya mazoezi ya pamoja ya jeshi

UKWELI KUHUSU MZEE MAJUTO, NA TETESI ZA KUFA