Arsenal yaichapa Huddersfield Town 5-0



Arsenal kwa sasa ipo nafasi ya nne na alama 28


Image captionArsenal kwa sasa ipo nafasi ya nne na alama 28

Arsenal imeweza kutakata vilivyo ikiwa nyumbani baada ya kuichapa Huddersfield Town 5-0 katika mchezo ambao Arsenal ilitawala kila idara.
Magoli ya Arsenal yamepachikwa na Alexandre Lacazette, Olivier Giroud akiingia nyavuni mara mbili, Alexis Sánchez na Mesut Özil.
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema ni faraja kupata alama tatu muhimu hususan wakati huu ambapo timu zinacheza michezo mingi.
Kwa upande wa David Wagner anayekinoa kikosi cha Huddersfield ametaja matokeo hayo kuwa mabaya na kuongeza kuwa ligi ya EPL ni ngumu kwani kila timu ina uwezo wa kushinda.
Kwa matokeo hayo Arsenal inapanda mpaka nafasi ya nne ikiwa na alama 28.

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi