Benevento wavunja rekodi ya Manchester United

Benevento


Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBenevento walikuwa tayari wamevunja rekodi ya kuwa na mwanzo mbaya zaidi Serie A

Klabu ya Benevento nchini Italia imevunja rekodi ya Manchester United ya kuwa klabu iliyoanza msimu vibaya zaidi katika ligi mojawapo kati ya ligi tano kuu za soka Ulaya.
Hii ni baada ya klabu hiyo kulazwa 2-1 muda wa ziada na Sassuolo.
Limbukeni hao wa Serie A wameshindwa mechi zao 13 za kwanza kwenye msimu na hivyo wakavunja rekodi ya United ambao walishindwa mechi 12 mwanzo wa msimu wa 1930-31.
Alessandro Matri aliwaweka Sassuolo kifua mbele lakini Samuel Armenteros akasawazisha kabla ya Gaetano Letizia alioneshwa kadi nyekundu upande wa Benevento.
Domenico Berardi alipoteza penalti upande wa Sassuolo kabla ya Federico Peluso kuwafungia bao la ushindi.
Benevento, ambao walifanikiwa kurejea Serie A mtawalia, walidhani wangepata alama yao ya kwanza ya msimu pale mkwaju wa penalti wa Berardi ulipogonga mwamba na kukosa kuingia.
Matumaini yao yalivunjwa dakika ya 94 Peluso alipofunga bao kwa kichwa.
United walishushwa daraja kutoka Ligi Kuu msimu wa 1930-31, msimu ambao walishindwa mechi saba pekee kati ya 42 walizocheza.
Walishindwa mechi 12 za kwanza msimu huo.
Benevento walikuwa tayari wamevunja rekodi ya kuwa na mwanzo mbaya zaidi Serie A na kuipita rekodi ya Venezia walioshindwa mechi tisa 1949-50.

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi