Chama tawala cha Zimbabwe ZANU - PF kumshtaki Mugabe

Rais Robert Mugabe


Haki miliki ya pichaAFP
Image captionRais Robert Mugabe akihutubia taifa Jumapili usiku

Mtandao wa Twitter unaofuatilia taarifa za vyombo vya habari nchini Zimbabwe unaripoti kuwa Kiongozi wa chama tawala Cha ZANU PF anaamini mchakato wa kumshtaki Bwana Mugabe utaendelea kama ilivyopangwa Jumanne , wakati ambapo chama bunge linatarajiwa kukaa. 
Hii ni kama muda wa makataa uliowekwa wa kujiuzulu kwake ambao ni Jumatatu saa sita adhuhuri utakwisha kabla Bwana Mugabe hajajiuzulu
Halikuwa tangazo ambalo baadhi ya waZimbabwe walilisubiri. Bwana Mugabe bado ni rais na haijawa wazi ikiwa bunge sasa litaanza mchakato wa kumshitaki.

Raia wa ZimbabweHaki miliki ya pichaAFP
Image captionRaia wa Zimbabwe wakirekodi hotuba ya kujiuzulu kwake

Watu wa Zimbabwe walikuwa wanatarajia kusikia mugabe akijiuzulu kulingana na madai yao.
Baadhi ya wale waliokusanyika kufuatilia hotuba yake kwenye vilabu waliiambia BBC kuwa wamekatishwa tamaa na kutojiuzulu kwa rais Mugabe.
Hata hivyo hali ya imeendelea kuwa tulivu katika maeneo mengi ya Zimbabwe, huku wengi waliendelea kusubiri mchakato utakaofuata.
Duru kutoka ndani ya mazungumzo ya hatma ya Mugabe zimeiambia BBC kuwa Mugabe mwenye umri wa miaka 93 alikuwa amekubali kuondoka madarakani , lakini baadae akabadili mawazo yake 
Jeshi linatarajiwa kuwa na mkutano na waandishi wa habari Jumatatu asubuhi pamoja na Muungano wa Wapiganaji waliopigania Uhuru wa Zimbabwe. 

Katika hotuba yake ya kwanza kwa taifa tangu jeshi lichukue madarakwa Jumatano, Mugabe hakujiuzulu na alisema kuwa ameazimia kuongoza kongamano lijalo la Zanu-PF.
Hatma yake sasa iko mashakani kwani kulingana na mbunge wa Zanu-PF Terence Mukupe anasema kongamano hilo ni mahala panopofaa kumuidhinisha kiongozi mpya anayependelewa na chama cha Zanu-PF

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi