CCM YATEUA WAGOMBEA SITA WA UENYEKITI WA WILAYA ZA KICHAMA



Chama cha Mapinduzi (CCM) kimefanya uteuzi wa majina ya wagombea wa uenyekiti wa wilaya sita za kichama.


Wilaya hizo ni Moshi Mjini, Hai, Siha, Makete, Musoma Mjini na Musoma Vijijini.


Taarifa kwa umma iliyotolewa na CCM jana Jumatatu Novemba 20,2017 imesema Kamati Kuu ya chama hicho kwa niaba ya Halmashauri Kuu imeteua majina ya wagombea katika wilaya ya Hai ambayo ni ya Abdulah Mriri, Magai Maganda na Justice Masawe.


Kwa Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro walioteuliwa ni Justice Mkita, Wilfred Mossi na Humfrey Nnko, huku Wilaya ya Moshi Mjini wateule ni Absalom Mwakyoma, Joseph Mtui, Faraji Swai na Alhaji Omar Amin Shamba.


Taarifa hiyo iliyosainiwa na Katibu wa NEC ya CCM, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole imesema kwa Wilaya ya Makete wateule ni Aida Chengula, Mwawite Njajilo na Onna Nkwama; Wilaya ya Musoma Mjini ni Robert Sylvester, Magiri Maregesi, Amina Nyamgambwa na Daud Misango.


CCM imesema wateule wa Musoma Vijijini ni Gerald Kasonyi, Kananda Hamisi Kananda na Nyabukika Bwire Nyabukika.


Polepole katika taarifa hiyo amesema Kamati Kuu imeagiza mikutano mikuu ya uchaguzi ya wilaya za Makete, Musoma Vijijini na Musoma Mjini ifanyike Novemba 25 na 26,2017.


Kwa wilaya za Moshi Mjini, Hai na Siha mikutano hiyo itafanyika Desemba Mosi na 2, 2017.

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi