Real Madrid yabanwa mbavu, Barcelona yajikita kileleni ‘La Liga’
Klabu ya Real Madrid jana usiku imelazimishwa sare ya bila kufungana na mahasimu wao klabu ya Atletico Madrid kwenye mchezo wa Ligi kuu nchini huu ‘La Liga’.
Mechi hiyo iliyokuwa na ushindani mkubwa ilionekana timu zote kutoshana nguvu kwani kipindi cha kwanza Madrid walionekana kutawala mchezo huku Atletico wakitawala kipindi cha pili.
Hii inakuwa ni mara ya kwanza Real Madrid kutoka sare tasa ya bila goli ugenini kwa mechi 35 iliyocheza chini ya Kocha Zinedine Zidane.
Kwaupande mwingine watani wao wa jadi, FC Barcelona hao walipata ushindi mnene wa goli 3-0 dhidi ya klabu ya Leganes na kuifanya klabu hiyo kujikita kileleni kwa alama 10 zaidi ya klabu za Madrid na Atletico.
Comments
Post a Comment