Waandamanaji wapiga kambi nje ya makao ya Mugabe

Waandamanaji nchini Zimbabwe wameelekea katika afisi ya rais Mugabe ili kumtaka kujiuzulu.


Image captionWaandamanaji nchini Zimbabwe wameelekea katika afisi ya rais Mugabe ili kumtaka kujiuzulu.

Waandamanaji nchini Zimbabwe wameelekea katika afisi ya rais Mugabe ili kumtaka kujiuzulu.
Maandamano hayo yanajiri kufuatia furaha ilioonekana miongoni mwa raia baada ya jeshi kuingilia kati na kumzuia rais Mugabe kwa muda nyumbani kwake siku ya Jumatano.
Wanajeshi katika ikulu ya Whitehouse walioonekana wakiwarudisha nyuma waandamanaji.
Jeshi liliingilia kati baada ya rais Mugabe kumfuta kazi makamu wake wa urais , akionyesha ishara za kutaka mkewe kumrithi.

Waandamanaji wakiunga mkono jeshi
Image captionWaandamanaji wakiunga mkono jeshi

Bwana Mugabe , mwenye umri wa miaka 93 ameiongoza Zimbabwe tangu ilipojipatia uhuru kutoka kwa Uingereza 1980.
Jeshi limehakikisha kuwa anaendelea kukaa katika makoa yake huku likidai kujadiliana naye na kwamba litatangaza kwa wananchi matokeo ya mazungumzo hayo hivi karibuni.
Mkutano wa siku ya Jumamosi unaungwa mkono na jeshi na wanachama wa chama cha Zanu -PF.

Waandamanaji wakimtaka rais Mugabe kujiuzulu wengi wakibeba mabango yakumtaka ang'atuke mamlakaniHaki miliki ya pichaEPA
Image captionWaandamanaji wakimtaka rais Mugabe kujiuzulu wengi wakibeba mabango yakumtaka ang'atuke mamlakani

Wapiganiaji wa uhuru ambao hadi kufiki mwaka uliopita walikuwa watiifu kwa rais Mugabe pia wanasema kwamba rais Mugabe anafaa kung'atuka mamlakani.
Kiongozi wa shirika hilo amewataka raia kuelekea katika makao ya rais Mugabe. 
Nje ya ikulu ya rais kuna baadhi ya watu walioketi chini ili kuonyesha pingamizi yao mbele ya majeshi, huku kiongozi wa upinzani Morgan Tsvangirai akihutubia umati mkubwa.

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi