EPL: Klabu gani ina wakati mgumu zaidi msimu wa Krismasi?


Football fan at ChristmasHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Ilichukua siku 87 kucheza mechi 11 za kwanza Ligi ya Premia.
Lakini mechi 11 zinazofuata zitachezwa katika siku 47 pekee.
Kila moja kati ya klabu zilizo kwenye Ligi Kuu itacheza mechi nne wakati wa sikukuu - mechi moja zaidi ya msimu uliopita.
Msimu uliopita, kila klabu ilikuwa na wiki ya kupumzika kabla ya mechi za Boxing Day isipokuwa Everton.
Mwaka huu, Leicester City watacheza mechi nne - kati ya 23 Desemba na 1 Januari - kipindi cha saa 213.
West Ham, nao watacheza mechi zao nne kwa mwendo wa aste aste kiasi, saa 294 na dakika 45.

Arsene WengerHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMsimu huu klabu ya Arsene Wenger ina nafuu zaidi ya klabu nyingine

Hii ni baada ya mechi yao ya Mkesha wa mwaka Mpya dhidi ya Tottenham kuhamishwa hadi 4 Januari kwa sababu za kiusalama.
Hilo limewapa karibu siku tatu za ziada za kupumzika.
Je, mpangilio kwa klabu mbalimbali ukoje?

Pamoja na Arsenal, mabingwa watetezi Chelsea pia wana mpangilio mwema wa mechi.
Watafaidi kutokana na kuhamishwa kwa mechi yao siku ya Mwaka Mpya hadi tarehe 3 Januari.
Viongozi wa ligi Manchester City pia watakuwa na wakati mzuri wa kupumzika kuliko klabu nyingine, ingawa watakuwa wenyeji wa Watford tarehe 2 Januari. Wageni wao hata hivyo watakuwa wamepumzika siku moja zaidi tangu mechi yao itakayotangulia.
Upande ule mwingine wa ligi, Brighton, Burnley na Bournemouth wote watahitajika kucheza emchi zao katika kipindi cha saa 215 - saa 21 chini ya muda wa wastani wa mechi za kipindi hicho ligini ambao ni saa 236.
Manchester United na Newcastle United pia wana mechi zilizofuatana kwa karibu.
Ni klabu mbili pekee - Huddersfield Town na Stoke City - ambazo hazijakuwa na mechi hata moja ambayo imehamishwa tarehe au kusongezwa muda.
Wachezaji watazidiwa?
Wachezaji na mameneja wa klabu zinazocheza Ligi Kuu ya England wamekuwa wakilalamika kwa muda mrefu kuhusu mpangilio wa mechi Desemba.
Januari waka huu, meneja wa Crystal Palace wakati huo Sam Allardyce alikosoa mpangilio huo baada ya timu yake kushindwa nyumbani na Swansea City.
Hata hivyo, kuna ushahidi unaoonyesha kwamba uwezo wa wachezaji huwa hauathiriwi na uchovu kipindi hiki cha mechi nyingi.
Kwa mujibu wa shirika la takwimu za michezo la Opta, kwa kawaida wachezaji huongeza kiwango chao cha uchezaji - kwa umbali wanaosafiri uwanjani na pia mitimko wanayofanya kwenye mechi - kipindi hiki.

Hakuna ushahidi wowote wa kuonyesha kwamba idadi ya magoli yanayofungwa na wachezaji wakati huo hupungua kutokana na uchovu wa wachezaji.
Katika misimu mitatu iliyopita, mechi zinazochezwa Krismasi na Januari huwa na idadi sawa ya magoli kwa wastani kwa kila mechi (2.7) sawa na mechi za nyakati hizo nyingine za msimu.
Makombora ya jumla kwa kila mechi (25.5 majira ya baridi ukilinganisha na 25.8 nyakati hizo nyingine) ukilinganisha na makombora yanayolenga goli kwa kila mechi (8.4 Desemba na Januari ukilinganisha na 8.5) pia hayana tofauti kubwa.
Suala la iwapo wachezaji huathiriwa na kipindi hicho baadaye kwenye msimu ni jambo ambalo limesalia kuwa mjadala.
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp akizungumzia mechi za Krismasi mwaka 2016 alisema: "Kila mtu anashangaa ni kwa nini England huwa haifanikiwi sana na michuano mbalimbali.
"Jiulize klabu nyingine zote (Ulaya) huwa zinafanya nini wakati huo. Huwa na miguu yao kwenye makochi wakitazama mechi za England."
Meneja wa England Gareth Southgate hata hivyo ameuliza iwapo wachezaji wake pengine wanaweza kufaidi kutokana na mapumziko Krismasi.

Si wachezaji na mameneja pekee wanaotatizwa na mechi za kipindi hicho - kuna mashabiki pia
Mashabiki wa Newcastle watasafiri mbali zaidi kwa mechi za Krismasi - takriban maili 964.
Tottenham mashabiki wao nao watasafiri maili 896 - mara tatu zaidi ya umbali wa mashabiki wa Manchester United (maili 288 ) na mara tano zaidi ya mashabiki wa Burnley (maili 160). 

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi