Trump: China na Urusi ndio washindani wakubwa wa Marekani

Trump


Image captionRais Trump

Rais Donald Trump ametangaza mkakati wa kitaifa wa usalama katika utawala wake ambao unaangazia vipaumbele vya kwanza vya Marekani.
Mkakati huo umesisitiza ukuaji wa kiuchumi na usalama wa taifa hilo kwa kuweka sheria kali za kulinda mipaka na kuwa na jeshi imara.
Katika hotuba yake,rais Trump ametaja kuwa China na Urusi ni washindani wanaopinga ushawishi wa Marekani katika ngazi ya kimataifa.
Licha ya kuwa Marekani inaongoza kwa kuwa na jeshi lenye nguvu lakini bado wapinzani wake wa kisiasa na kiuchumi wanahangaika duniani kote ili kuitoa katika mstari.
Huku ikiwa inakabiliwa na makundi ya kigaidi ,mitandao ya wahalifu na watu wengine ambao wanachochea vurugu na uovu.
Aidha mkakati huo unajumuisha ujenzi wa ukuta katika mpaka wa Mexico, kuimarisha sheria za uhamiaji na kusitisha mpango wa kutoa viza za bahati nasibu.
Trump pia aliwakosoa pia Marais waliopita wa Marekani akisema wameshiriki katika ujenzi wa mataifa ya nje badala ya kuendeleza taifa lao . 

Comments

Popular posts from this blog

GOR MAHIA MABINGWA WA SPORTPESA SUPER CUP 2017, SASA KUKIPIGA NA EVERTON JULAI 13

Marekani na Korea Kusini wafanya mazoezi ya pamoja ya jeshi

UKWELI KUHUSU MZEE MAJUTO, NA TETESI ZA KUFA