Katibu mkuu wa CUF Maalim seif hamad ametuma salamu za lambi lambi kwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania DR.John Pombe Magufuli.
"Natuma salamu zangu za rambirambi kwa ndugu, jamaa na marafiki wa waathirika wote na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Na kwa wale waliojeruhiwa nawatakia uponaji wa haraka ili warejee katika majukumu yao ya kawaida, na tunawaombea marehemu wote Mwenyenzi Mungu awapumzishe mahala pema peponi", amesema Maalim Seif.
Pamoja na hayo Maalim Seif amesema anaungana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kulaani shambulio hilo, na kuitaka nchi ya Congo kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo, na kuwachukulia hatua wale waliohusika.
“Tunaungana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kulaani shambulio hilo ambalo ni sawa na uhalifu wa kivita, na kuitaka DRC Congo kufanya uchunguzi kuhusu shambulio hilo na wahusika wote kuchukuliwa hatua stahiki na kuwajibishwa", amesema Maalim Seif.
Hapo Jana imetolewa taarifa kuwa askari 14 wa Tanzania wa kulinda amani nchini Kongo wameuawa, huku 44 wakiwa majeruhi, 8 miongoni mwao wakiwa mahututi, na wawili hawajulikani walipo.
Comments
Post a Comment