Mataifa ya Kiarabu yataka kuiwekea Marekani vikwazo vya Kiuchumi
Jana Jumamosi kulishuhudiwa ghasia katika mji wa Nablus, West Bank
Mataifa ya kiarabu yameitaka Marekani kubatilisha uamuzi wake wa kuitambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israeli.
Kwa njia ya taarifa walioitoa kwa kauli moja kwenye mkutano wao Mjini Cairo- Misri, muungano huo umesema kuwa hatua hiyo ni hatari na ni ukiukaji wa sheria za kimataifa, na litaitumbukiza mataifa ya mashariki ya kati katika ghasia mbaya.
Mawaziri kwenye mkutano huo, sasa wanaiomba jamii ya kimataifa kutaja Mashariki mwa Jerusalem kama makao makuu ya Palestina.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Lebanon, Gebran Bassil, amesema kuwa mataifa ya kiarabu, yanafaa kufikiria hatua ya kuiwekea Marekani vikwazo vya kiuchumi, ili kuizuia kuhamishia makao makuu ya Israeli hadi Jerusalem, kutoka Tel- Aviv.
Bwana Bassil, amesema kuwa, hatua za kidiplomasia na kisiasa, zinafaa kuchukuliwa, kisha kufuatiwa na vikwazo vya kiuchumi na kifedha.
Kumeshuhudiwa tena ghasia katika ukanda wa Gaza na maeneo ambayo yanashikiliwa na Israeli, Magharibi mwa mto Jordan.
Comments
Post a Comment