Mwanamke aliyejaribu kuwauza watoto wake pacha akamatwa Nigeria
Mwanamke mmoja amekamatwa baada ya madai kuwa alijaribu kuwauza watoto wake pacha wenye umri wa mwezi mmoja nchini Nigeria.
Ameshtaki kwa kuhusika katika bishara ya kuuza watoto lakini polisi wanasema kuwa mashtaka zaidi yataongezwa.
Mwanamke huyo alikamatwa wakati akijaribu kuuza watoto wake wasicha kwa dola 980 kwa mnunuzi ambaye aliwajulisha polisi.
Visa vya kuuzwa watoto wa kupangwa vimekuwa tatizo kwa muda mrefu chini Nigeria.
Alipohojiwa mwanamke huyo alisema kuwa changamoto za kifedha zilisababisha afanye hivyo.
Nigeria ni mzalishaji mkuwa wa mafuta lakini asilimia kubwa ya watu milioni 170 wanaishi kwenye umaskini.
Mwaka 2013 wasichana wajawazito 17 na watoto 11 waliokolewa wakati polisi walivamia "kiwanda cha watoto" katika jimbo la Imo
Miaka miwili baada ya sakata hiyo, mwanamke mwingine alishikwa akipokuwa akijaribu kumuuza mtoto wake kwa dola 90 katika jimbo la Cross River.
Comments
Post a Comment