Mwanamke aliyemuua mume wake ili aishi na mpenzi wake India
Wapenzi wiwili nchini India wamekamatwa kwa kumuua mume wa mwanamke na kisha kujaribu kumfanyia upasuaji wa kubadilisha sura mwanamume mpenzi ili aweze kuchukua mahala pake,
Tindi kali ilimwagwa kwenye uso wa mwanamume, mpenzi wa mwanamkea, katika shambulizi lililopangwa, huku wapenzi hao wakipanga kusema kuwa sura yake ilikuwa imebadilika baada ya upasuaji.
Lakini ndugu wa bwana wa mwanamke aligundua mpango huo alipofika hospitalini.
Alitoa malalamiko yake kwa polisi ambao walifanya uchunguzi wa vidole na kugundua njama huyo.
Mke, Swati Reddy amekamatwa. Polisi waliiambia BBC kuwa watamkamata pia mpenzi wake, Rajesh Ajjakolu mara atakapotibiwa majeraha yake na kuruhusiwa kuondoka hospitalini.
Bwana Sudhakar Reddy anadaiwa kuuliwa usiku wa tarehe 26 Novemba na mwili wake kutupwa siku iliyofuatia. Hadi sasa mwiwi huo bado haujapatikana.
Polisi wanasema kuwa mwanamke huyo amekiri kuwa walimuua mume wake.
Rajeshi Ajjakolu alilazwa hospitalini tarehe 28 Novemba huku Bi Reddy akiwajulisha familia ya mume wake kuhusu shambulizi la tindi kali.
Polisi wanasema kuwa wazazi wa Bw. Reddy waliamini kuwa mwanamume ambaye alikuwa akipata matibabu alikuwa ni mtoto wao na kulipa hadi dola 7,758 kama bili ya hospitali.
Njama hiyo haikugunduliwa hadi tarehe 9 mwezi Disemba, wakati ndugu yake Reddy, alifika hospitalini humo na kuwajulisha polisi aliposhuku kuwa mwanamume huyo hakuwa ndugu yake.
Comments
Post a Comment