Zaidi ya watoto laki nne wapo hatarini kutokana na utapiamlo DRC

Wazazi na watoto wakiwa katika msururu wa kupata huduma ya afya DRC


Image captionWazazi na watoto wakiwa katika msururu wa kupata huduma ya afya DRC

Shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia watoto UNICEF limeonya kuwa zaidi ya watoto laki nne walio chini ya miaka mitano wanakumbwa na utapiamlo mkubwa nchini DRC.
Linasema kuwa watoto hao wanaweza kufa ndani ya miezi michache kutoka sasa kama juhudi za haraka hazitachukuliwa.
UNICEF inasema mgogoro uliopo kwenye jimbo la Kasai,na kudorora kwa shughuli za kilimo ni sababu kubwa ya tatizo hilo.
Hali ya usalama kwa baadhi ya maeneo ya Kongo DRC imezorota kutokana na vikundi vinavyoipinga serikali ya Kabila kufanya mashambulizi kwa wananchi na hivyo kukwamisha baadhi ya shughuli muhimu za kijamii.

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi