Japan Yapeleka mtambo wa kutibua makombora ya Korea Kaskazini Yatakayorushwa katika Kisiwa cha Marekani.


Japan imepeleka mtambo wa kutibua makombora magharibi mwa taifa hilo kufuatia tishio la Korea Kaskazini kwamba itarusha kombora la masafa marefu katika kisiwa cha Guam nchini Marekani.

Mtambo huo kwa Jina PAC3 (Patriot Advanced Capability-3) umepelekwa katika eneo la shimane, Hiroshima na Kochi ambapo Pyongyang( Korea Kaskazini )  inasema kombora lake litapaa kabla ya kuanguka katika maji ya Guam.
Jeshi la kulinda baharini la Japan limeripotiwa kutuma mtambo wa kutibua makombora katika bahari ya Japan likiwa na mfumo wa kufuatilia makombora ya masafa marefu.

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Jinsi ya kutengeneza SABUNI ya kipande YA KUGANDISHA

Alexander Lacazette Shujaa wa Arsenal