UN yataka mapigano kusitishwa Syria kupisha misaada

Raia wengi wapo katika hali mbaya kwa kukosa chakula na huduma nyingine muhimu


Image captionRaia wengi wapo katika hali mbaya kwa kukosa chakula na huduma nyingine muhimu

Umoja wa Mataifa umetoa wito kusimamishwa kwa muda mapigano katika mji wa Ragga nchini Syria, kuruhusu idadi ya raia waliopo katika eneo hilo la mapigano kuondoka.
Mkuu wa misaada ya kibinadamu nchini Syria, Jan Egeland, anasema mji wa Raqqa yawezekana kwa sasa ni moja kati maeneo hatari duniani na kutaka hatua za haraka kuchukuliwa ili kutoa mwanya kwa raia kutoroka katika eneo hilo.
Amesema kuwa wapiganaji wa Islamic State wanatumia kundi la raia waliobaki kama kinga ya kivita.
Hata hivyo idadi hiyo ya raia wapatao 25,000 kwa wamekwama ndani ya mji huo huku kukiwa na mfululizo wa mashambulizi ya anga kwa juma moja lililopita.

Ragga unatajwa kuwa miongoni mwa miji hatari zaidi duniani
Image captionRagga unatajwa kuwa miongoni mwa miji hatari zaidi duniani

Shirika la kimataifa la Amnesty linasema mamia ya watu wameuawa tangua mashambulizi hayo yalipoanza katika mji wa Raqqa mwezi june mwaka huu.
Wapiganaji wa IS wanatuhumiwa na umoja wa mataifa kwamba wanatumia raia kama kinga yao katika mapigano hayo.
Marekani na Muungano wa vikosi vya Syria, Kiarabu na Kikurdi wanajaribu kuukomboa mji huo kutoka mikononi mwa wapiganaji wa Islamic state.

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi