Hatari yaongezeka kwa mlima wa volkano kulipuka Bali

Maafisa wanasema mlma huo wa volkano umekuwa ukitoa moshi mkubwa mfululizo


Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMaafisa wanasema mlma huo wa volkano umekuwa ukitoa moshi mkubwa mfululizo

Mamlaka nchini Indonesia imetangaza hali ya tahadhari kubwa kufuatia kuwepo dalili za kutokea mlipuko mkubwa wa Volcano katika mlima wa Agung. 
Uwanja wa ndege wa kipekee katika kisiwa hicho maarufu cha utalii cha Bali umefungwa.
Majivu na moshi wa Volcano hiyo imefikia urefu wa zaidi ya mita 3000 juu ya mlima huo hali iliyosababisha giza.
Mlima huo uitwao Agung ulirusha majivu mengi na kutandaza mvuke na moshi mwingi mara ya pili katika kipindi cha wiki moja. 
Maafisa wamehimiza na kuwasaidia maelfu ya wakaazi na watalii kulihama ene hilo na kwenda kwingine.
Mwaka 1963 mlima huo ulilipuka na kusababisha vifo vya takriban watu 1,600.

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi