Gordon Reid atinga nusu fainali michuano ya Tennis Masters

Gordon Reid anatarajiwa kupanda kwenye viwango vya kimataifa hivi karibuni


Image captionGordon Reid anatarajiwa kupanda kwenye viwango vya kimataifa hivi karibuni

Muingereza Gordon Reid ameshinda mchezo wake wa pili katika mashindano ya walemavu ya Tennis Masters na kujiweka katika nafasi nzuri ya kuingia kwenye hatua ya nusu fainali itakayopigwa mjini Loughborough.
Baada ya kupoteza mbele ya bingwa Joachim Gerard siku ya Jumatano, Reid amemshinda Nicolas Peifer wa Ufaranda kwa seti 3-6 6-4 6-3.
Muingereza mwenzake Andy Lapthorne nae pia amefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kumchapa Heath Davidson wa Australia kwa seti 6-2 7-5.
Alfie Hewett naLucy Shuker walipoteza michezo yao.
Hewett, namba mbili kwa ubora duniani kwa upande wa wanaume, alipangwa kucheza na Shingo Kunieda wa Japan lakini alipoteza kwa seti 2-6 6-4 6-2 baada ya kuumia bega.

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi