Tundu Lissu: Kushambuliwa kwangu kulichochewa na siasa Tanzania

Mwanasheria kuu wa chama upinzani Chadema nchini Tanzania Tundu Lissu, ambaye amekuwa akipokea matibabu Nairobi tangu alipopigwa risasi na watu wasiojulikana jijini Dodoma mwezi Septemba, amesema anaamini kushambuliwa kwake kulihusiana na siasa nchini humo.
Akizungumza na BBC, mbunge huyo wa Singida Mashariki amelilaumu Bunge la nchi hiyo akisema halijachukua hatua zozote kumsaidia tangu kulazwa kwake hospitalini.
Makamu wa Rais wa Tanzania Bi Samia Suluhu alimtembelea hospitalini mapema wiki hii.
Bw Lissu amesema anaendelea kupata nafuu vyema.
Juhudi za BBC za kuwasiliana na msemaji wa Bunge la Tanzania kuhusu tuhuma za Bw Lissu hazijafua dafu.
Amezungumza na mwandishi wa BBC John Nene.

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi