Mshindi wa Turner Prize ni mzawa wa Zanzibar

Profesa Lubaina Himid ni mzaliwa wa Zanzibar


Image captionProfesa Lubaina Himid ni mzaliwa wa Zanzibar ,mshindi wa Turner Prize

Profesa Lubaina Himid ni mzaliwa wa Zanzibar ambaye ni mtanzania ametangazwa kuwa mshindi wa 'Turner Prize 2017'katika tuzo kubwa za Sanaa nchini Uingereza. 
Majaji wamempa Tuzo kwa maonesho matatu yaliyofanyika Oxford, Bristol na Nottingham ambapo waliisifu kazi yake ambayo inaangazia Afrika duniani kote pamoja na ubunifu wa mtu mweusi jambo ambalo wameliita namna nzuri ya ubunifu. 

Tuzo za Turner
Image captionTuzo za Turner

Profesa Himid ambaye ni mwanamke wa kwanza mweusi na mtu mwenye umri mkubwa zaidi kuwahi kutwaa Tuzo hiyo amesema atatumia tuzo ya fedha ya dola elfu thelathini na tatu ($33,000) alizozipata kuwasaidia wasanii wachanga kuweza kuonesha kazi zao.

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Jinsi ya kutengeneza SABUNI ya kipande YA KUGANDISHA

Alexander Lacazette Shujaa wa Arsenal