Man United, Basel zasonga mbele klabu bingwa ulaya
Michezo nane ya kwanza ya hatua ya mwisho ya makundi ya klabu bingwa barani ulaya imechezwa usiku huu na jumla ya timu kumi na mbili tayari zimefuzu kwa hatua ya kumi na sita bora.
Katika kundi A Manchester United, wameibuka vinara wa kundi hilo kwa kuwa na alama 15,baada ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya CSKA Moscow, nao Fc Basel wamesonga mbele kwa kwa kuwa na alama 12 baada ya ushindi wa 2-0 ugenini dhidi ya Benfica.
Katika kundi B Bayern Munich wamewachapa Paris Saint Germain, kwa kichapo cha goli 3-1 na Celtic wakafungwa 1-0 na Anderlecht hiyo Psg na Bayern ndio wanafuzu kwa hatua inayofuata huku Celtic, wakishiriki michuano ya Europa ligi.
Atletico Madridi wameshindwa kusonga mbele baada ya kukubali sare ya goli 1-1 na Chelsea ugenini hivyo wanakwenda kushiriki Europa ligi, As Roma, wakawatungua Qarabag Fk, kwa bao 1-0, hivyo katika kundi C ni As Roma na Chelsea ndio wamesonga mbele.
Barcelona, wamemaliza hatua ya makundi bila ya kufungwa baada ushindi wa 2 - 0 Sporting CP, na kumaliza vinara kwa jumla ya alama 14, wakifuatiwa na Juventus wenye alama 11 baada ya kuwachabanga Olympiacos kwa mabao 2-0
Comments
Post a Comment