Trump matatani ukatili wa kijinsia

Rais Donald Trump matatani ukatili wa kijinsia.


Image captionRais Donald Trump matatani ukatili wa kijinsia.

Wanawake watatu wamemtuhumu rais Donald Trump kwamba aliwafanyia ukatili wa kijinisa miaka iliyopita kabla hajawa rais.Hivyo baraza la Congress kumchunguza trump kutokana na kashfa hizo.
Wanawake walioibua kashafa hiyo dhidi ya Rais Trump ni Jessica Leeds, Samantha Holvey, na Rachel Crooks wamesema kuwa rais Trump bila ridhaa yao alikuwa akiwa shika shika,kuwabusu kwa nguvu na ukatili mwingine.Lakini hata hivyo ikulu ya white house imesema kuwa madai ya wanawake hao si ya kweli.
"Rais alikwisha elezea wazi wazi kashfa hizi,katika mikutano yake ya kampeni hata kabla hajawa rais.Na tunaamini kuwa madai haya yalikwisha jibiwa kwa mfumo huo."Sarah Huckabee Sanders
Rachel Crooks katika madai yake dhidi ya kashfa hiyo ya rais Trump,anasema kuwa yeye alilazimishwa kupigwa busu na rais Trump nje ya lift ya majengo ya ghorofa za Trump enzi hizo akiwa na miaka 22. Japo kuwa mkasa huo ulitokea miaka mingi iliyopita,anasema bado Trumpa anapaswa kuchukuliwa hatua.
Mwanamke mwingine anayemtuhumu rais Trump ni mlimbwende wa mwaka 2006 Bi Samantha Holvey ambaye anasema ,Trump alihudhuria mashindano hayo na alikuwa anawakagua mwilini kama vile nyama inavyokaguliwa buchani,na amesema kuwa hana nia ya kumchukulia hatua rais Trump bali anaweka wazi kile alichofanyiwa.
Rais Trump tangu aingie madarakani amekuwa akiandamwa na kashfa mbali mbali zikiwemo za kisiasa na zile zinahusiswa na biashara zake.

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi